TAWHIYD
    Tawhiyd

Qur'aan

Sunnah

Fiqhi

Makala

Nasiha Ya Ijumaa

Dua na Adhkaar

'Aqiyda-Tawhiyd

Vitabu

Darsa za Wanawake

    Sikiliza

Qur'aan

Mawaidha

Dua

Nashiyd

    Tizama

Video

 » Makala na Mengineyo  

Adhabu ya Kaburi

Anasema Sheikh Ibn Uthaymiyn (Mwenyezi Mungu amrehemu):

‘Zipo dalili nyingi sahihi zinazoelezea juu ya Adhabu ya kaburini. Mwenyezi Mungu anasema:

“Adhabu ya Motoni wanadhihirishiwa (makaburini mwao) asubuhi na jioni . Na siku ile kitakapotokea Kiama (kutasemwa) “Waingizeni watu wa Firauni katka adhabu kali zaidi

Al Muumin (Ghafir - 46)

Hii ni dalili katika Qurani kuwa Firauni na watu wake wanadhihirishiwa adhabu asubuhi na jioni kabla ya Siku ya Kiama. Kwa sababu aya inaendelea kusema : ‘Na siku ile kitakapotokea Kiama ‘ na maana yake ni kuwa hiyo adhabu iliyotajwa ya kudhihirishiwa Moto asubuhi na jioni ilikuwepo kabla ya Siku ya Kiama

 

Na katika hadithi nyingi sahihi Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) amesema:

‘Muombeni Mwenyezi Mungu akukingeni na adhabu ya MotoWakasema: ‘Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu na adhabu ya MotoAkasema: ‘Muombeni Mwenyezi Mungu akukingeni na adhabu ya KaburiWakasema: ‘Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na adhabu ya Kaburini

Muslim – 2867

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) pia alisema juu ya Muislamu :

‘Anapanuliwa kaburini mwake kiasi cha upeo wa macho yake

Bukhari – 1374

Dalili kama hizi ziko nyingi sana, na haijuzu mtu kuzikanusha kwa ajili ya matamanio ya nafsi yake.

Adhabu ya kaburini ni ya kiroho na si jambo linalohusu mwili, na hii ndiyo sababu ikawa imani juu yake ni katika mambo ya ghaibu. Na hali ya mambo katika maisha ya Barzakh hayawezi kukisiwa kwa hali ya maisha yetu ya hapa duniani.

Isitoshe, adhabu ya Kaburini na neema zake anayadiriki maiti peke yake na wanadamu wengine hawawezi kuyaona wala kuhisi au kuyadiriki. Mfano wake ni sawa na mfano wa mtu anapoota usingizini. Anaota kuwa anakwenda anarudi, anapigwa anapiga. Anajiona yupo mahali penye nafasi kubwa na mara nyingine anajiona yupo penye nafasi ndogo iliyodhikika. Anayaona yote wakati walio karibu yake hawayaoni wala hawayahisi

(Mwisho wa maneno ya Sheikh Ibn Uthaymiyn

 

Kama ilivyoeleza aya ya adhabu wanayopata Firauni na watu wake hadi siku ya kiama, pia zipo aya nyingi zinazoelezea juu ya neema wanayopata Waumini na pia juu ya adhabu wanayopata makafiri wanapotolewa roho zao, na baada ya kutolewa roho zao.

Mwenyezi Mungu anasema:

‘Na laiti ungeliona Malaika wanapowafisha wale waliokufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao na kuwaambia; Ingojeni adhabu ya moto.

Hayo ni kwa sababu ya (maasi) yake yaliyofanya na mikono yenu. Na hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulunu waja (waka

Al Anfal – 50-51

Na akasema juu ya Mashuhadaa:

‘Wala usiwadhani wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu (maiti) bali wahai wanaruzukiwa kwa Mola wao.

Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila Zake na wanawashangilia wale ambao hawajajiunga nao, walio nyuma yao ya kwamba haitokuwa hofu juu yao wala hawatohuzunika

Aali Imran -169-170

Aya kama hizi za kuadhibishwa makafiri pale wanapotolewa roho zao na baada yake, pamoja na neema wanazopata Waislamu wanapotolewa roho zao na baada yake pamoja na Adhabu wanayopata Firauni na watu wake ni nyingi sana, jambo linalotufanya tusiweze kukanusha juu ya adhabu ya kaburini zilizotajwa wazi wazi na Mtume wa Mwenyezi Mungu katika hadithi zake nyingi sahihi tulizozitaja na tusizozitaja.

Wallahu taala aalam

Wassalaam alaykum wa Rahmtullahi wa Barakatuh