Anasema
Allaah
سبحانه
وتعالى
}}الَّذِينَ
آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلاَوَتِهِ
أُوْلَئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ{{
{{Wale
tuliowapa Kitabu, wakakisoma kama ipasavyo kusomwa, hao ndio
kweli wanakiamini}}
Al-Baqarah:121
Na
Anasema Allaah
سبحانه وتعالى
}}إِنَّ
الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ
وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً
يَرْجُونَ
تِجَارَةً لَّن تَبُورَ{{
}}
لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ
إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ{{
{{Hakika wale
wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakasimamisha
Swalah, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika
Tulivyowaruzuku, hao hutaraji biashara isiyododa
(isiyoanguka)}}
{{Ili Yeye
Awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na Awazidishie kutokana na
fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye
shukrani}} Faatwir:
29-30
1) Mtu
bora kabisa ni mwenye kusoma na kuifundisha
عن
عثمانَ بن
عفانَ رضي الله
عنه أنَّ
النبيَّ صلى
الله عليه
وسلّم قالَ
)) خَيرُكُم
مَنْ تعَلَّمَ
القُرآنَ
وعَلَّمَه))
صحيح
البخاريِّ
Imetoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan
رضي الله عنه
kwamba
Mtume
صلى
الله عليه وآله وسلم
amesema ((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur'aan kisha
akaifundisha))
Al-Bukhariy
2) Thawabu
mara mbili kwa mwenye kuisoma kwa mashaka
عن عائشة رضي
الله عنها
أنَّ النبي
صلى الله عليه
وسلّم قال))
الماهرُ
بالقرآن مع
السَّفرةِ الكرامِ
البررة،
والذي
يقرأ
القرآنَ
ويتتعتعُ فيه
وهو عليه
شاقٌّ له
أجرانِ))
البخاري ومسلم
Imetoka kwa 'Aisha
رضي الله عنها
kwamba Mtume صلى
الله عليه وآله وسلم
amesema,
((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur'aan atakuwa pamoja na
Malaika Waandishi wa Allaah
watukufu wacha Mungu, na yule ambaye anaisoma Qur'aan kwa
mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara
mbili))
Al-Bukhariy na Muslim
3) Watu wa
Qur'aan ni watu bora kwa Allaah
سبحانه وتعالى
عن
أنس رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله
عليه وسلم (( إن لله تعالى أهلين من الناس .
قالوا : يا
رسول الله من هم ؟ قال : هم أهل
القران أهل
الله وخاصته
(( صحيح
الجامع
Imetoka
kwa Anas
رضي الله عنه
kwamba Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
amesema ((Allaah
سبحانه وتعالى
Anao watu wa aina mbili, wakamuuliza, ewe Mjumbe wa Allaah,
nani hao? Akasema, hao ni watu walioiandama Qur'aan na ni
watu waliokuwa bora kabisa wa Allaah))
Sahiyh Al-Jaami'
4)
Tofauti ya anayeisoma na asiyeisoma Qur'aan
عن أبي
موسى
الأشْعَريِّ
رضي الله عنه
أنَّ النَّبي
صلى الله عليه
وسلّم قالَ ((مثلُ
المؤمنِ
الَّذِي
يقرأ
القرآنَ
مَثَلُ الأتْرُجَّةِ
ريحُها طيبٌ
وطعمُها
طيّبٌ، ومثَلُ
المؤمِن
الَّذِي لاَ
يقرَأ
القرآنَ كمثلِ
التمرة
لا
ريحَ لها
وطعمُها حلوٌ ))
البخاري ومسلم
Kutoka kwa Abu Musa Al-Ash'ariy
رضي الله عنه
kwamba Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
amesema ((Mfano wa Muumini ambaye anayesoma Qur'aan ni
kama tunda la Utrujjah harufu yake nzuri na ladha yake
nzuri. Na mfano wa Muumini asiyesoma Qur'aan mfano wake
kama tende zisizokuwa na harufu lakini zina ladha tamu))
Al-Bukhariy na Muslim
5) Thawabu
kwa kila herufi moja
عن
عبدالله بن
مسعودٍ رضي
الله عنه أن
النبيَّ صلى
الله عليه
وسلّم قال: ((
من
قَرأ حرفاً
من
كتاب الله
فَلَهُ
به
حَسَنَةٌ،
والحسنَةُ
بعشْر
أمْثالها، لا
أقُول الم حرفٌ ولكن
ألفٌ حرفٌ ولاَمٌ
حرفٌ
وميمٌ حرفٌ))
رواه الترمذي.
Imetoka kwa 'Abdullahi Bin Mas'uud
رضي الله عنه
kwamba Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
amesema, ((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah
atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na
thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja,
bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni
herufi moja))
At-Tirimidhiy
6) Kiombezi
Siku ya Qiyaamah
عن أبي
أمَامةَ رضي
الله عنه أنَّ
النبيَّ صلى
الله عليه
وسلّم قال
)) اقْرَؤوا
القُرآنَ
فإنه يأتي
يومَ القيامةِ
شفيعاً
لأصحابهِ
((
مسلم
Imetoka kwa Abu Umaamah رضي
الله عنه
kwamba Mtumeصلى
الله عليه وآله وسلم
amesema ((Someni Qur'aan kwani itakuja siku ya Qiyaamah
ikimuombea
mwenye
kuisoma))
Muslim
7) Qur'aan
humnyanyua mtu na humdhalilisha mwingine
قال
عمر رضي الله عنه : أما إن نبيكم صلى الله عليه
وسلم قد قال : (( إن الله يرفع بهذا الكتاب أقواماً
ويضع
به آخرين ))
صحيح مسلم
Imetoka kwa 'Umar
رضي الله عنه
ambaye amesema, Mtume wenu amesema
((Allaah Atawanyanyua
baadhi ya watu kwa kitabu hiki (Qur'aan) na Atawadhalilisha
wengine kwa kitabu hiki))
Muslim
8) Qur'aan
humpandisha mtu daraja ya Pepo
عن
عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال : قال رسول
الله صلى الله عليه وسلم (( يقال لصاحب القران
اقرأ
و ارتق ورتل كما كنت ترتل في الدنيا فإن
منزلتك عند آخر آية تقرؤها )) .
(صحيح الجامع
Imetoka kwa 'Abdullah bin 'Umar
رضي الله عنهما
kwamba Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
amesema ((Huambiwa rafiki wa Qur'aan (Aliyeiandama Qur'aan)
soma na panda (juu katika daraja za Pepo)
na
uisome kwa 'Tartiyl' (utaratibu na utungo) kama ulivyokuwa
ukiisoma (kwa Tartiyl) ulipokuwa duniani, kwani makazi yako
ni pale utakapofika katika aya ya mwisho utakayoisoma))
Sahiyh
Al-Jaami'i
9) Mwenye
kuhifadhi Qur'aan hutangulia kaburini
عن جابر رضي الله عنه كان رسول الله صلى الله
عليه وسلم يجمع بين الرجلين من قتلى أحد في
ثوب واحد
ثم يقول : أيهم أكثر أخذاً للقرآن ؟ فإذا
أشير إلى أحدهما قدمه في اللحد .
(صحيح البخاري)
Imetoka kwa Jaabir
رضي الله عنه
kwamba alikuwa Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
akiwakusanya watu wawili waliokufa katika vita vya Uhud
katika nguo moja kisha anauliza, ((Nani katika hao mwenye
Qur'aan zaidi? Anapojulishwa mmoja kati ya hao, humtanguliza
kaburini))
Al-Bukhariy
10) Kuteremka Malaika kwa Utulivu na Rahma kwa wanaosoma
Qur'aan
عن
أبى هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله
عليه وسلم قال ((ما اجتمع قوم
في بيت من بيوت
الله يتلون
كتاب الله ويتدارسونه فيما بينهم
إلا نزلت عليهم
السكينة وغشيتهم الرحمة
وحفتهم الملائكة وذكرهم الله فيمن عنده)) . صحيح
مسلم
Imetoka kwa Abu Hurayrah
رضي الله عنه
kwamba Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
amesema ((Hawakusanyiki pamoja watu katika miongoni mwa
nyumba za Allaah wakisoma kitabu cha Allaah, na
wanafundishana baina yao, ila huwateremkia utulivu na
hufunikwa na rahma na Malaika huwazunguka na Allaah
Anawataja mbele ya aliokuwa nao)) Muslim
11) Kuhifadhi na kujifunza maana yake ni bora kuliko
mapambo ya dunia
عن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال: خرج رسول الله
صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال((أيغدو أحدكم
كل يوم إلى بطحان
العقيق, فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم? فقلنا يا
رسول الله نحب ذلك قال : أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيتعلم أو يقرأ آيتين
من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين,
وثلاث خير له من ثلاث , وأربع خير
له من أربع , ومن أعدادهن من الإبل))
رواه مسلم وغيره
Imetoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir
رضي الله عنه
ambaye amesema, Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alitujia wakati tulikuwa katika Suffah akauliza, kuna yeyote
miongoni mwenu anayetaka kwenda
soko
la But-haan-Al-'Aqiyq na akapata humo ngamia wawili (wa
thamani kabisa wa kike) bila ya kutenda dhambi au kukata
undugu? Tukajibu kwamba sote tunapenda kufanya na kupata
hivyo. Kisha akasema, basi aende mmoja wenu msikitini
akajifunze au asome aya mbili katika kitabu cha Allaah
سبحانه وتعالى
basi akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia (wa thamani kabisa
wa kike). Na aya tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na aya
nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa
aya kwa ngamia ))
Muslim
12) Mwenye kuhifadhi Qur'aan huvalishwa taji
عن
أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله
صلى الله عليه وسلم
((يجيء القرآن يوم القيامة فيقول:
يا رب حله, فيلبس تاج
الكرامة ثم يقول: يا رب زده, فيلبس حلة الكرامة, ثم يقول: يا رب ارض عنه
فيرضى عنه
فيقول: اقرأ وارق ويزاد بكل آية حسنة)) رواه
الترمذي والحاكم
وصححه
الألباني
Imetoka kwa Abu Hurayrah
رضي الله عنه
ambaye amesema, Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
amesema, ((Qur'aan itakuja siku ya Qiyaamah na itasema, Ewe
Mola, Mpambe (Mwenye kuhifadhi Qur'aan) kisha atavalishwa
taji, kisha (Qu'raan) itasema Ewe Mola, muongezee, kisha
huyo mtu atavishwa nguo ya heshima, kisha itasema (Qur'aan)
Ewe Mola Ridhika naye, Allaah
سبحانه وتعالى
Ataridhika naye. Kisha ataambiwa, soma na panda, atapokea
thawabu zaidi za mema kwa kila aya (atakayosoma) ))
At-Tirmidhy na Al-Haakim na kaisahihisha Albaniy
Allaahumma Tujaalie Tuwe Wenye
Kuiandama Qur'aan Ili Utulipe Fadhila hizi Ya Rabb.
Tutaendelea Inshaa-Allaah Ijumaa ijayo. Tumuombe Allaah
سبحانه وتعالى
Atunufaishe kwa yale tunayojifunza na Atuajaalie miongoni
mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo
njema.
Tunawaombea wote Ijumaa hii iwe ya kheri na baraka nyingi.
Aamiyn