|
Faida zake:
1)
Wanaoswali
Qiyaamul-Llayl
wameandaliwa
Pepo.
Anasema
Allaah
سبحانه وتعالى
}}تَتَجَافَى
جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا
وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ{{
}} فَلَا
تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ
جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {{
{{Mbavu zao zinaachana na vitanda
kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa
kutokana na tulivyowaruzuku}}
{{Nafsi yoyote haijui waliyo
fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya
yale waliyo kuwa wakiyatenda}} As-Sajdah 16-17
Aya hizi
zinambashiria Pepo Muislamu mwenye kuhangaika na
kujitahidi kusimama kuswali usiku
na mwenye kutoa mali yake kwa ajili ya Allaah
سبحانه وتعالى,
zinambashiria pepo ambayo imejaa mazuri Aliyoyaficha Allaah
سبحانه وتعالى
kwa ajili yao, mazuri ya kupendeza yatakayodumu milele
ambayo hajapata mtu kuyaona kwa sababu ya
vitendo vyao vizuri
walivyovifanya vilifichika na Allaah
سبحانه وتعالى
Anaficha thawabu zao.
ففي صحيح
البخاري
وغيره عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صلى
الله عليه وسلم قال)):
قال الله تعالى:
أعددت لعبادي الصالحين ما لا عين
رأت، ولا أذن سمعت، ولا خطر على قلب بشر، فاقرؤوا إن شئتم
فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ
أَعْيُنٍ جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
((
Al
Bukhari na wengineo wamesimulia kwamba Abu Hurayrah
رضي الله amesema kwamba, Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
amesema:
(("Allaah
سبحانه وتعالى
Amesema, Nimewatayarishia waja Wangu wema yale ambayo macho
hayajapata kuona, wala masikio hayajapata kusikia, na wala
hayajapata kupita katika akili ya mtu, kwa hiyo someni
mkipenda
فَلاَ
تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ
جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa
katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale
waliyo kuwa wakiyatenda )) As-Sajdah
16-17
Vile vile
Allaah
سبحانه وتعالى Ametaja
Wacha Mungu watakaokuwa Peponi na yale waliyokuwa
wakiyafanya, na mojawapo ni kukesha usiku kwa kufanya ibada,
}}إِنَّ
الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ{{
}}
آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ إِنَّهُمْ
كَانُوا قَبْلَ ذَلِكَ مُحْسِنِينَ{{
}}
كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا
يَهْجَعُونَ{{
}}
وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُون{{
}}وَفِي
أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ{{
{{Hakika Wacha Mungu watakuwa
katika Mabustani na chemchem}}
{{Wanapokea aliyowapa Mola wao
Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya
mema}}
{{Walikuwa wakilala kidogo tu
usiku}}
{{Na katika mali
yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiyeomba}}
Adh-Dhaariyaat: 15-19
2) Sifa
za Waja wa Ar-Rahmaan
}}وَعِبَادُ
الرَّحْمَنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا
وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا
{{
}} وَالَّذِينَ
يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا{{
{{Na waja wa Ar Rahman Mwingi wa
Rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga
wakiwasemeza hujibu: Salama!}}
{{Na wale wanaokesha kwa ajili ya
Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama}}
Al-Furqaan: 63-64
3)
Sio sawa na wengine
}}لَيْسُواْ
سَوَاء مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَآئِمَةٌ يَتْلُونَ
آيَاتِ اللّهِ آنَاء اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ{{
{{Wote hao si sawa sawa. Miongoni
mwa Watu wa Kitabu wamo watu waliosimama barabara, wanasoma
Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu}}
Al-'Imraan: 113
}}أَمَّنْ
هُوَ قَانِتٌ آنَاء اللَّيْلِ سَاجِدًا
وَقَائِمًا يَحْذَرُ
الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ قُلْ
هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ
يَعْلَمُونَ
وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا
يَتَذَكَّرُ أُوْلُوا
الْأَلْبَابِ{{
{{Je! Afanyae
ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari
na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi...Sema:
Eti watakuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Hakika
wanaokumbuka ni watu wenye akili}}
Az-Zumar:9
4) Nyakati
za kughufuriwa
Kama Anavyosema Allaah
سبحانه وتعالى:
}}الصَّابِرِينَ
وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ
وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالأَسْحَارِ{{
{{Wanaosubiri,
wanaosema kweli, na watiifu, na wanaotoa sadaka, na
wanaoomba maghfira kabla ya alfajiri}}
Al-'Imraan
17
Vile vile:
((عن
أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول
الله صلى الله عليه وسلم قال: ينزل
ربنا تبارك وتعالى كل ليلة إلى السماء
الدنيا حين يبقى ثلث الليل الآخر
فيقول:
من يدعوني فأستجيب له؟ من
يسألني فأعطيه؟ من
يستغفرني فأغفر له))
رواه
الجماعة.
((Imetoka
kwa Abu Hurayra
رضي الله عنه
kwamba Mtume
صلى الله عليه وسلم ِAmesema:
Allaah
سبحانه وتعالى
Huteremka kila siku katika mbingu ya dunia (mbingu ya
kwanza) inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani
ananiomba Nimtakabalie? Nani Ana shida nimtekelezee? Nani
ananiomba maghfira Nimghufurie?))
Imesimuliwa na Jama'a
5) Siha
kwa mwili
((عليكم
بقيام الليل فإنه دأب الصالحين
قبلكم، وقربة إلى الله تعالى، ومكفرة
للسيئات، ومنهاة عن الإثم،
ومطردة للداء
عن الجسد ))
رواه أحمد والترمذي وصححه
الألباني
((Shikamaneni na
kusimama (kuswali) usiku kwani ni tabia/adabu za waja wema
kabla yenu, na kujikurubisha kwa Allaah
سبحانه وتعالى
, na ni kafara ya maovu, na ni kinga ya dhambi, na ni
kiondosho cha maradhi katika mwili))
Ahmad na At-Tirmidhiy na
kaisahihisha Albaniy
6) Nyakati ya kukubaliwa dua'a
Amesema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
:
((ان في الليل لساعة لا يوافقها رجل مسلم يسأل
الله تعالي خيرا من امر الدنيا
و الاخرة، الا اعطاه اياه،
وذلك
كل ليلة))
رواه
مسلم
((Hakika katika
usiku kuna saa ambayo mja anapomuomba Allaah
سبحانه وتعالى
kheri katika mambo ya dunia au Akhera ila (Allaah) Humpa
kheri hizo, na hivyo ni kila usiku))
Muslim
7) Usharifu (Utukufu) wa Mu'mim
Kama alivyosema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم:
((أتاني جبريل فقال: يا محمد، عش ما
شئت فإنك ميت، وأحبب من شئت فإنك
مفارقه، واعمل ما شئت فإنك
مجزي به، واعلم
أن شرف المؤمن قيامه بالليل، وعزه استغناؤه عن الناس ))
رواه
الحاكم والبيهقي وحسنه المنذري والألباني
((Amenijia Jibriyl akasema: Ewe
Muhammad ishi upendavyo bila shaka wewe ni maiti (utakufa),
na mpende umtakaye bila shaka utafarikiana naye, na tenda
unavyopenda lakini ujue utalipwa kwa vitendo hivyo, na
tambua kwamba utukufu wa Muumin ni Qiyaamul-Llayl, na
heshima yake ni kujitosheleza Na watu))
Al Haakim na Al
Bayhaqiy, na Al Mundhiriy na Albaaniy wamesema ni Hadiyth
Hasan
8) Husnul-Khaatimah (Mwisho Mwema)
((من
قام بعشر آيات لم يُكتب من
الغافلين، ومن قام بمائة آية كتب من القانتين، ومن قام بألف
آية كتب من
المقنطرين
((
رواه أبو داود وصححه
الألباني (والمقنطرون هم الذين لهم قنطار من الأجر)
((Atakayesimama (usiku) na aya
kumi hatoandikiwa katika miongoni mwa walioghafilika, na
atakayesimama kwa aya mia ataandikiwa ni miongoni mwa
wanyenyekevu, na atakayesimama kwa aya Alfu ataandikwa
miongoni mwa wenye mirundi)) Abu Dawuud na
amesahihisha Albaniy (Maana ya mirundi ni wale walio na
mrundi wa thawabu)
9)
Uso hung'ara kwa Nuru
يقول الحسن البصري
رحمه الله :
"
لم أجد من العبادة شيئا أشد من الصلاة
في
جوف الليل" فقيل
له :
ما بال المجتهدين من أحسن الناس وجوها
فقال: "لأنهم خلوا بالرحمن
فألبسهم من نوره"
Anasema
Hasan Al Baswry Mwenyeezi Mungu Amrehemu:
"Sijapata
kuona ibada iliyo nzito kama Swalah katika kiza cha usiku".
Akaulizwa, Vipi wale watu wajitahidio wenye nyuso nzuri
kabisa? Akajibu,
"kwa sababu
wamejitenga (wamejifaraghisha na) Na Ar-Rahmaan, basi Naye
Akawavisha Nuru Yake" .
Sababu za
kukuwezesha kuamka Qiyaamul-layl
a) Usile
na kunywa hadi ukashiba sana usiku.
b) Usijitaabishe
sana mchana kwa yasiyo na faida.
c) Usiache
'Qaylulah' (kulala kidogo mchana) kwani inasaidia kuamka
usiku.
d) Usifanye
maasi kwani yanamzuia mtu kuamka Qiyaamul- layl.
e) Safisha
moyo wako kutokana na uhasidi, chuki na waislamu wenzako.
f) Fikiria
mauti na usiwe na matumaini ya kuishi sana.
g) Tambua
fadhila zake.
Tutaendelea
Inshaa-Allaah Ijumaa ijayo. Tumuombe Allaah
سبحانه وتعالى
Atunufaishe kwa yale tunayojifunza na Atuajaalie ni miongoni
mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo
njema.
Tunawaombea wote
Ijumaa hii iwe ya kheri na baraka nyingi. Aamiyn
|