|
Shukrani zote ni za Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)
Ni
katika baraka zake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa Muislamu
Kumuwezesha kufunga mwezi wa Ramadhani na kuutumia wakati
wake wa usiku kwa Swalah. Ni mwezi ambao ndani yake amali
njema huzidishwa malipo na watu hupandishwa daraja (vyeo).
Ni wakati ambao Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Huwaachia huru
baadhi ya watu kutokana na Moto. Kwa hivyo Muislamu ni
lazima ajitahidi sana kufanya mambo mema katika mwezi huu;
ni lazima afanye hima katika kuutumia wakati wa uhai wake
wenye ibada. Kuna watu wangapi ambao wamenyimika katika
mwezi huu kutokana na maradhi, mauti au kukosa maelekezo
mema.
Muislamu ni lazima ajitahidi sana (kufanya matendo mema)
katika wakati wake wote ndani ya mwezi huu; anayo majukumu
yasiyoweza kuepukika juu ya watoto wake, kuwalea vizuri na
kuwatunza vyema, kuwahimiza kufanya kila aina ya vitendo
vyema na kuwafanya waendelee kukuwa navyo – kwa sababu
mtoto hukulia katika mwenendo ambao wazazi wake wamemzoeza.
Katika wakati wa siku hizi zilizobarikiwa, baba na mama wana
nafasi adhimu ya kufanya yenye manufaa, na tunaweza kutoa
ushauri ufuatao kwa wazazi:
1 -
Kuzifuatilia Swawm za watoto wao na kuwapa moyo wale
wanaoshindwa kufanikisha.
2 –
Kuwahimiza kuhusu Swawm halisi inavyotakiwa, na sio tu
kujizuilia kula na kunywa, lakini ni njia ya kufikia kwenye
Kumcha Mwenyezi Mungu (Taqwa), na hiyo ni nafasi maalumu ya
kusamehewa madhambi na kulipwa malipo mema.
Imesimuliwa kutokana na Abu Hurayrah kwamba Mjumbe wa Allah
( Rehma na Amani Zimshukiye Juu Yake) alishuka kutoka juu
ya minbar na akasema :
“Aamiyn, Aamiyn, Aamiyn.” Akaulizwa, “ Ewe
Mjumbe wa Allah, kwa nini umefanya hivyo?” Akasema, “Jibriil
alinambia, ‘amekula khasara yule ambaye Ramadhaan imemfikia
na akawa hakusamehewa dhambi zake, na nikasema , ‘Aamiyn’.
Baadaye akasema, ‘amekula khasara yule ambaye ameishi na
hali ya kuwa amewaona wazazi wake mpaka wakawa vizee, mmoja
wao au wote wawili, lakini ikawa hajaingia peponi,’ na
nikasema, ‘Aamiyn’. Baadaye akasema, ‘amekula khasara yule
ambaye wakati unapotajwa ikawa yupo na asikutakie Rehma juu
yako,’ na nikasema, ‘Aamiyn’.”
Imepokelewa na Ibn Khuzaymah, 1888; at-Tirmidhiy, 3545;
Ahmad, 7444; Ibn Hibbaan, 908. Angalia Sahiih al-Jaami’,
3501.
3 –
Wafundishe (watoto) adabu nzuri na namna ya kula, kwa mfano
kula kwa kutumia mkono wa kulia na kunywa kwa kutumia mkono
wa kulia na kuchukua chakula kutoka mbele ya nafasi zao
(wasichukue upande wa mwengine); wakumbushe kwamba kufanya
israfu katika chakula ni Haraamu na ni madhara kwa mwili.
4 –
Usiwaachie kutumia wakati mrefu katika kula futari ikafikia
hadi wakakosa Swalah ya jamaa ya Maghribi.
5 –
Wakumbushe kuhusu hali za masikini na mafaqiri ambao
hawawezi kumudu hata tonge ya chakula angalau wakaondosha
moto wa njaa yao; Wakumbushe hali za wale wote ambao aidha
huhama au hupigania Jihadi kwa ajili ya kutaka ridhaa ya
Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika sehemu zote.
6 –
Mikusanyiko hii (ya mwezi wa Ramadhaan) inatoa nafasi nzuri
ya kuwajumuisha jamaa pamoja na kuthibitisha mshikamano wa
koo. Mazoea
kama haya yapo katika baadhi ya nchi, na vile vile ni nafasi
nzuri ya kupatanisha na kutengeneza uhusiano uliovunjika
baina ya jamaa.
7 –
Inamsaidia mama (kupata nafasi nzuri ya) kutayarisha
chakula, kusafisha na vilevile kukiweka chakula muweko
unaostahiki.
8
–Wawahimize watoto kuswali Swalah ya Taarawiyh na kujiandaa
kwa ajili ya hiyo Swalah kwa kutokula sana na kujiweka
tayari kwa wakati ili kwenda msikitini.
9 –
Kwa kuzingatia Daku, wazazi ni lazima wawafundishe watoto
baraka za daku na kwamba daku humpa mtu nguvu ya kufunga.
10 –
Waruhusu kuwa na wakati wa kutosha kabla ya Swalah ya
Alfajir ili kwa wale ambao hawakuswali Swalah ya Witri
waweze kufanya hivyo kwenye wakati ule, na vile vile kwa
wale wanaochelewesha Swalah zao hadi wakati wa mwisho wa
usiku, waweze kusali na pia kila mmoja aweze kuomba du’aa
kwa Mwenyezi Mungu vyovyote vile mtu apendavyo.
11 –
Pawepo mazingatio ya kwenda msikitini kwa ajili ya Swalah ya
jamaa ya Alfajir, kwa wale wanaowajibika kufanya hivyo.
Tunaona watu wengine ambao huamka katika mwisho wa usiku kwa
ajili ya kula daku, huwa wanarejea tena kulala na kupuuza
(kupitwa) na Swalah ya Afajir.
12 –
Ilikuwa ni kawaida ya Mtume (Rehma na Amani Zimshukie Juu
Yake) katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani kukesha
usiku na kuwaamsha watu wake. Hii inamaanisha kwamba familia
ni lazima izingatie kufanya jitihada kwenye wakati huu
adhimu (wenye baraka) ili kufanya matendo ambayo
yanamridhisha Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), huenda mtu
Akatukuzwa na Kupandishwa daraja (za Amali zake njema). Kwa
hivyo Mume ni lazima awaamshe Mkewe na Watoto wake ili
kuyafanya yale ambayo yatawapelekea kuwa karibu na Mola Wetu
(Subhaanahu wa Ta’ala).
13 –
Hutokezeya wakati mwengine ikawa kuna watoto wadogo katika
nyumba ambao wanahitaji kupewa moyo ili waweze kufunga, kwa
hivyo baba ni lazima awahimize kuamka kwa ajili ya kula
daku, na vile vile awape moyo kwa kuwasifu na kuwatunukia
pindi wakimaliza mwezi mzima au hata wakifikisha nusu yake,
na vinginevyo (robo ya mwezi au wiki moja).
Imesimuliwa kwamba Ar-Rubayyi’ bint Mu’awwidh alisema:
Ilikuwa asubuhi ya mwezi wa ‘Ashuraa’ Mtume (Rehma na Amani
Zimshukie Juu Yake) alipeleka habari kwenye vijiji vya
Answaar akasema,
“ Yeyote aliyeamka bila ya kufunga, basi na
asile kwa muda wote uliobakia kwa siku ile, na yeyote
aliyeanza kufunga basi na aendelee na Swawm yake.” Akasema
(bibi huyu): Tulikuwa tukifunga na kuwafungisha watoto wetu,
[na tulikuwa tukiwachukua msikitini] na tukiwatengenezea
vitu vya kuchezea vya sufi , ili ikiwa mmoja wao atalilia
chakula basi humpa kile kitu cha kuchezea (ili kimliwaze)
mpaka ufike wakati wa kuftari.
Imepokelewa na al-Bukhaariy, 1859; Muslim,
1136 – Maneno ya kwenye mabano yamepokelewa na Muslim.
An–Nawawiy amesema:
Hadiyth hii inaonyesha kwamba ni lazima
tuwafunze watoto wetu juu ya kufanya matendo ya ibada na
tuwaendeleze ili wakulie nayo, ijapokuwa wao hawahesabiwi
(kwa ajili ya umri wao kuwa mdogo).
Al-Qaadhi amesema: Imesimuliwa kutokana na ‘Urwah kwamba
pale wanapokuwa wao wanaweza kufunga basi huwa ni lazima
juu yao kufunga. Hili ni kosa ambalo halina uthibitisho wa
hadiyth sahihi, “Kalamu huondoshwa
kutokana na (mambo) matatu: kutoka mtoto anapozaliwa mpaka
afikiapo kuwa msichana/mvulana …….” Na Allah ni Mjuzi
Zaidi.
Sharh
Muslim, 8/14
14 –
Ikiwa inawezekana, baba na mama ni lazima wende na watoto
wao kwenye ‘Umrah (Hijja ndogo) wakati wa Ramadhaan, na
kufanya hivyo ni manufaa juu yao na katika maisha ya
baadae, kwa nafsi zao wenyewe wazazi na familia yao pia.
Ibada ya Umrah katika mwezi wa Ramadhaan ina
ujira sawa na Hijja. Ni bora kwenda kufanya ‘Umrah katika
wakati wa mwanzo wa mwezi wa Ramadhaan ili kuepuka
misongamano ya watu.
15 – Mume asimbebeshe kazi nyingi kupita
uwezo wake mkewe kwa kupika vyakula vingi. Watu wengi
huuchukulia mwezi wa Ramadhaan kuwa ni mwezi wa kubuni
vyakula na vinywaji (vya kila aina) na huwa wanazama zaidi
kwenye hayo.
Hii
inapunguza thamani ya uzuri wa mwezi huu na inakwenda
kinyume na madhumuni ya kufunga, ambapo ni kufikia Ucha
Mungu (Taqwa).
16 –
Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi wa Qur-aan, kwa hivyo tunashauri
kila familia iwe inajikusanya pamoja kwa ajili ya kusoma
Qur-aan.
Baba aifundishe familia yake namna ya kusoma
na maana ya ayah za Qur-aan. Katika mkusanyiko huo huo kuwe
kunafundishwa (aidha kwa njia ya usomaji wa vitabu juu ya)
adabu za kufunga. Katika mwezi wa Ramadhaan Allah (Subhaanahu
wa Ta’ala) Huwawezesha wengi katika wanavyuoni na watafutao
elimu kuandika vitabu ambavyo hutumika kwa ajili ya
mihadhara na kufundishia; vitabu hivyo hugaiwa katika sehemu
thelathini ambapo kila sehemu huwa na mada isomwayo kwa
siku moja na huleta manufaa kwa kila mtu.
17 – Ni lazima wahimizwe kuutumia wakati wao
kuwapitia majirani na wenye shida (kuhitaji).
Imesimuliwa kwamba Ibn ‘Abbaas Amesema:
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ( Rehma na Amani Zimshukie Juu
Yake) alikuwa ni Mkarimu sana kwa watu, na alikuwa katika
kiwango kikubwa zaidi cha ukarimu wakati wa mwezi wa
Ramadhaan.
Wakati Malaika Jibriyl alipomjia. Alikuwa akimjia kila
usiku akimzoeza Qur-aan pamoja naye. Mjumbe wa Allah (Rehma
na Amani Zimshukie Juu Yake) alikuwa Mkarimu sana kuliko
hata mvumo wa upepo.
Imepokewa na al-Bukhaariy, 6; Muslim, 2308.
18 –
Wazazi ni lazima wazikinge familia zao na watoto wao
kutokana na kukaa muda mrefu wakati wa usiku na kuupoteza
muda katika matendo yasiyokuwa na manufaa, vitu vya
kumpumbaza mtu ni haramu? Waovu miongoni mwa watu katika
mwezi wa Ramadhaan huwa zaidi ni kishawishi kikubwa katika
kuchochea waliofunga ili wafanye vitendo vibaya na viovu,
usiku na mchana.
19 –
Ni lazima wakumbuke Mkutano wa Familia katika Pepo
ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika maisha ya Akhera, na
ni furaha kubwa kukutana huko wakiwa kwenye kivuli cha
Ufalme Wake ( Allah). Mikusanyiko hii ya Baraka katika
ulimwengu huu inaletwa kutokana na kumtii Allah
(Subhaanahu wa Ta’ala). Kufunga na Kuswali ni njia moja wapo
inayopelekea kupatikana furaha.
|