">
TAWHIYD
    Tawhiyd

Qur'aan

Sunnah

Fiqhi

Makala

Nasiha Ya Ijumaa

Dua na Adhkaar

'Aqiyda-Tawhiyd

Vitabu

Darsa za Wanawake

    Sikiliza

Qur'aan

Mawaidha

Dua

Nashiyd

    Tizama

Video

 » Mengineyo  

Hatari Ya Kuchelewa Kuomba Maghfira Na Tawbah

Muislam anapofanya maasi ni lazima atubie haraka iwezekanavyo kuonyesha kuwa ametambua makosa yake, na hapo ndipo atakapokuwa amedhamiria kwa nia safi ya kurudi kwa Mola wake kumuomba msamaha na kunyenyekea Kwake.

}}إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللّهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوَءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُوْلَـئِكَ يَتُوبُ اللّهُ عَلَيْهِمْ وَكَانَ اللّهُ عَلِيماً حَكِيماً{{

{{Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima}}

An-Nisaa 17

 

Kuchelewa kuomba Tawbah   huenda kusifae tena

Huenda mtu akaendelea kufanya madhambi hadi akafika wakati wa kukata tamaa ya kuishi na wakati wa kuiaga dunia umekaribia ndipo akatambua umuhimu wa kuomba tawbah kwa Mola wake, hapo tena atakuwa kachelewa kabisa na hapo tawbah yake itakuwa haina faida tena kama alivyosema Allaah  :سبحانه وتعالى   

}}وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّى إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الآنَ وَلاَ الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ أُوْلَـئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا{{

{{Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanao kufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu }}

 An-Nisaa 18

Mfano mzuri tunao katika Qur'aan  wa Fir'awn kama alivyofanya wakati anazama na hapo ndio akaona hana hila tena ndio akaomba tawbah, 

}}وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا حَتَّى إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لا إِلِـهَ إِلاَّ الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَاْ مِنَ الْمُسْلِمِينَ{{

{{Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea!}}   Yunus 90

Allaah سبحانه وتعالى Akamuuliza Fir'awn wakati anatapatapa na kuomba na kudai kuwa kaamini:

}}آلآنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ{{

{{Alaa! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni   mwa  mafisadi!}}  Yunus 91  

Kisha Akaikataa Tawbah yake katika hali hii:

}}فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ{{

{{Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu}} Yunus  92

Mtume صلى الله عليه وسلم vile vile hakuaacha  kutufahamisha hatari ya kuchelewa kuomba tawbah kama katika hadithi zifuatazo zinavyoonyesha

 

 Kuomba tawba kabla ya sakaraatil-maut   

((قال صلى الله عليه وسلم: إن الله يقبل توبة العبد ما لم يغرغر)) رواه أحمد والترمذي وصححه النووي

))Hakika Allaah سبحانه وتعالى huikubali toba ya mja wake kabla ya roho kufika kwenye mkoromo wa mauti))  Imesimuliwa na Ahmad na Kusahishwa na An-Nawawy

 

Na Kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi

((عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صل قال  : من تاب قبل أن تطلع الشمس من مغربها تاب الله عليه))        رواه مسلم

((Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema,  "Atakayetubu kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi, Allaah سبحانه وتعالى Atamkubalia toba yake"))  Muslim

 

Kabla ya moyo kupofuka wote  

Hatari nyingine ni kuwa huenda ikampofoa mtu moyo wake akawa hajali tena kufanya maovu na hata ikawa shida tena mtu huyo kupata uongofu , huwa haoni hasikii yumo katika maasi.  Hadithi ya Mtume صلى الله عليه  وآله  وسلم inasema kuhusu hili:

((عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: إن العبد إذا أذنب ذنباً نكت في قلبه نكتة سوداء ، فإذا تاب ونزع واستغفر صُقل قلبه ، وإن زاد زادت حتى تعلوا قلبه ، فذلك الران الذي ذكره الله عز وجل

 

  }}كَلاَّ بَلْ رَانَ عَلَى قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ  ({{ ( المطففين :)   رواه أحمد والترمذي وحسنه الألباني

 

((Imetoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه  Mja anapofanya dhambi, doa jeusi (kutu) huwekwa katika moyo wake.  Akiacha dhambi hiyo, na kuomba maghfira  na kutubu, moyo wake husafishwa ukawa msafi, lakini akirudia kufanya dhambi, doa (kutu)  huzidi kuenea  mpaka kufunika moyo wote na hiyo ndio 'Raan'  (kutu)  aliyosema Allaah سبحانه وتعالى  {{ Sivyo hivyo! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao (maovu) waliyokuwa wakiyachuma}} (Al-Mutaffifiin 14) ))

Imesimuliwa na Ahmad, At-Tirmidhi na Sheikh Albaani kasema ni hadithi Hassan