|
Anasema
Mtume (SAW) katika hadithi kwamba:
مثل البيت الذي يذكر الله فيه ،
والبيت الذي لا يذكر الله فيه مثل الحي والميت.
Mfano wa nyumba ambayo anatajwa Allah(SW) (kwa
kukumbukuwa) ndani yake na mfano wa nyumba asiotajwa
Allah(SW) ni sawa na mtu alie hai na maiti
Hatuna budi ndugu zangu waislamu kukumbushana
na kunasihiana kwamba nyumba zetu zijengwe kwa misingi ya
kuwa ni sehemu za ibada pia licha ya kuwa sehemu za
kujipumzisha na kujisitiri.
Tunatakiwa tuutumie vizuri wakati tupo
majumbani pamoja na familia zetu kwa
1.
Kumtaja Allah(SW) ,
2.
Kumkumbuka ikiwa ndani ya nyoyo zetu au
kwenye ndimi zetu.
3.
Kusali sala za sunna(za fardhi lazima
zisaliwe misikitini) .
4.
Kusoma/kusikiliza/kujifunza/kufundisha Quraan
5.
Kujifunza mambo mengi ya dini yetu kwa kusoma
vitabu vya kidini .
6.
Kujenga mazoea ya kutazama/kusikiliza kanda
za mawaidha na dvd za kiislamu
Vyenginevyo nyumba zetu ikiwa hazitajwi wala
kukumbukwa Allah(SW) zitakuwa kama alivyozielezea Mtume(SAW)
“maiti”. Hazina uhai kwa kukosekana utajo wa Allah(SW) ndani
yake na moja kwa moja kuingiliwa na shetani alielaaniwa na
kukimbiwa na malaika. Hivyo kupatikana ndani yake kila aina
ya uchafu na balaa ambalo kwa jinsi shetani anavyoyazaini na
kuyapamba huonekana kuwa ni mambo mazuri.
Hivyo ni wajibu kuzihuisha nyumba zetu na
kumtaja na kumkumbuka Allah(SW) kila tupatapo wasaa wa
kufanya hivyo.
Wabillahi Tawfiq
|