|
Mwezi huu mtukufu umejaa fursa ya kujichumia mengi ya kheri
ambayo thawabu zake huanzia tokea kumi hadi zaidi ya mia
saba pamoja na malipo maalum yatokayo kwa Allaah kwa
Mfungaji,
kama alivyosema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
((قال صلى الله عليه وسلم :
كل
عمل ابن آدم له الحسنة بعشر أمثالها إلى سبعمائة
ضعف . يقول الله عز وجل : إلا الصيام فإنه لي وأنا أجزي به ،
ترك شهوته وطعامه
وشرابه من أجلي، للصائم فرحتان ؛ فرحة عند فطره ، وفرحة عند
لقاء ربه، و لخلوف
فم الصائم أطيب عند الله من ريح المسك))
أخرجه
البخاري ومسلم
((Amesema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم, kila amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa
thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah
سبحانه وتعالى Anasema isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye
nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake na
maji yake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga atapata furaha
mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Mola
wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri
mbele ya Allaah
سبحانه وتعالى kuliko harufu ya misk))
Al-Bukhariy na Muslim
Kwanza
kabisa inatupasa tuanze mwezi huu mtukufu kwa kutia Nia
moyoni (si kuitamka) yenye Ikhlaas ambayo ndio msingi wa
kutaqabaliwa amali ya ibada yoyote, na ili kupata Ridhaa ya
Allaah
سبحانه وتعالى
kama Anavyosema:
}}وَمَا
أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ
الدِّينَ
حُنَفَاء وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ
وَذَلِكَ دِينُ
الْقَيِّمَةِ {{
{{Nao hawakuamrishwa kitu ila
wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu,
na washike Swalah, na watoe Zakah. Na hiyo ndiyo Dini
madhubuti}}
Al-Bayyinah: 5
Ifuatayo ni baadhi ya
milango ya kheri ambayo inampasa kila Muislamu ajitahidi
kuiingia na kutekeleza hizo amali njema katika mwezi huu
mtukufu wenye kheri na baraka nyingi ili kujichumia mema
mengi yatakayomfaa mtu akhera.
1) Swawm
kwa imani ili Kufutiwa madhambi
قال صلى الله عليه وسلم : (( من صام رمضان إيماناً و احتساباً
غفر له ما تقدم من
ذنبه )) أخرجه
البخاري ومسلم
Amesema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم ((Atakayefunga Ramadhaan kwa imaan na kutegemea malipo ataghufuriwa
madhambi yake yaliotangulia ))
Al Bukhariy na Muslim.
2) Qiyaamul-Layl
(Kusimama Usiku katika Swalah) Tarawiyh na Tahajjud
((قال صلى الله عليه وسلم : من قام رمضان إيماناً واحتساباً ،
غفر له ما
تقدم
من ذنبه ))
أخرجه البخاري ومسلم
((Amesema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم Atakayesimama (kwa Swalah ya usiku) kwa imani na kutaraji malipo,
ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) Al-Bukhariy na Muslim.
3) Sadaka
((قال صلى الله عليه وسلم: أفضل
الصدقة صدقة في رمضان ))
أخرجه الترمذي عن أنس
((Amesema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
Sadaka bora kabisa ni ile inayotolewa katika mwezi wa
Ramadhaan)) At-Tirmidhy kutoka kwa Anas
4)
Kumfuturisha
aliyefunga
((قال صلى الله عليه وسلم : من فطر صائماً كان له مثل أجره
غير أنه لا ينقص من
أجر
الصائم شيء ))
أخرجه أحمد والنسائي وصححه الألبان
((Amesema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
"Atakayemfuturisha aliyefunga, atapata ujira
kama
ujira wake bila ya kupungua chochote katika ujira wa yule
aliyefunga))
Ahmad, An-Nasaaiy na kasahihisha Sh Albani
Na Allaah
سبحانه وتعالى Anasema:
}}وَيُطْعِمُونَ
الطَّعَامَ عَلَى حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا{{
}}
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ
جَزَاء وَلَا شُكُورًا{{
}}
إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا{{
}}
فَوَقَاهُمُ اللَّهُ شَرَّ ذَلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ
نَضْرَةً وَسُرُورًا{{
}}وَجَزَاهُم
بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا{{
{{Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na
yatima, na wafungwa}}
{{Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu.
Hatutaki kwenu malipo wala shukrani}}
{{Hakika sisi tunaiogopa kwa
Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu}}
{{Basi Mwenyezi Mungu
Atawalinda na shari ya siku hiyo na Kuwakutanisha na neema
na furaha}}
{{Na Atawajazi Bustani za
Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyosubiri}}
Al-Insaan:
8-12
Vile vile kasema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم :
((
أيما مؤمن أطعم مؤمناً على جوع أطعمه الله من
ثمارالجنة ومن سقى مؤمناً على
ظمأ سقاه الله من الرحيق المختوم ))
رواه
الترمذي بسند حسن
.
((Muumin yeyote atakayemlisha Muumin mwenzake mwenye njaa,
Allaah Atamlisha katika matunda ya Peponi, na
atakayemnywisha mu'min mwenye kiu Allaah Atamnywesha kutoka
'Rahiyqul-Makhtuum' [Kinywaji safi
kilichofunikwa kwa kizibo madhubuti] )) At-Tirmidhiy kwa Sanad nzuri.
5) Kusoma
Qur'aan
sana na kujua maana yake
Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi
ulioteremshwa Qur'aan
kama Anavyosema Allaah
سبحانه وتعالى:
}}
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى
لِّلنَّاسِ
وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَان{{
{{Mwezi wa Ramadhaan ambao
imeteremshwa humo Qur'aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja
zilizo wazi za uongofu na upambanuzi}}
Al-Baqarah: 185
Kwa hiyo inampasa Muislamu
azidishe kusoma Qur'aan na ajitahidi kukhitimisha japo mara
moja katika mwezi huu
kama alivyokuwa akifanya Jibriyl
عليه السلام
wakati
akimfundisha Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
Qur'aan kila Ramadhaan. Vile vile Maswahaba na Salaf Swaalih
(Wema Waliopita) walikuwa wakijihimiza
sana kusoma Qur'aan mwezi huu.
'Uthmaan bin 'Affaan
رضي الله عنه alikuwa akikhitimisha Qur'aan kila siku mara moja. Na baadhi ya Salaf
wakikhitimisha katika Kisimamo cha usiku kila baada ya siku
tatu. Na wengineo kila siku saba, na wengine kila siku kumi.
Na walikuwa wakiisoma katika Swalah na nje ya Swalah.
6) Kukaa
kwa kumkumbuka Allaah baada Swalah ya Alfajiri hadi jua
litoke
((عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنه قال : من صلى
الفجر
في جماعة
ثم
قعد يذكر الله
حتى تطلع الشمس ثم صلى ركعتين كانت له كأجر حجة وعمرة
تامة تامة تامة) )
أخرج الترمذي صححه الألباني
.
((Imetoka kwa Anas kwamba Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم amesema, Atakayeswali Alfajiri katika Jama'ah kisha akakaa anamkumbuka
Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'a mbili,
atapata ujira
kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) Imetolewa na At-Tirmidhy na kaisahihisha Albani
(Kuswali Jama'ah
imesisitizwa kwa wanaume,
ama mwanamke anaweza naye kupata thawabu hizi sawa akiswali
nyumbani kwake)
Thawabu hizo ni katika siku za kawaida
ndugu Muislamu, seuze mwezi wa Ramadhaan? Nayo ni fadhila
ya siku moja tu, na ikiwa atatimiza kila wiki mara moja,
atakuwa ana thawabu za Hajj na 'Umrah mara nne kwa mwezi, na
akiendelea hivyo miezi yote kumi na mbili basi atakuwa na
thawabu za Hajj na 'Umrah mara 48 kwa mwaka. Yatakuwaje
malipo yake akitimiza kila siku? Na hii ni mojawapo ya neema
na uadilifu wa Allaah
سبحانه وتعالى
kwamba hata maskini asiyeweza kujilipia kwenda Hajj au 'Umrah
aweze kupata thawabu hizi akiwa nyumbani kwake, tena chumo
lenyewe hilo, lenye thawabu nyingi zenye kumshinda hata yule
mwenye uwezo wa mali, ni kwa muda wa usiozidi masaa mawili;
tokea Alfajiri hadi kuchomoza jua. Hizi ni neema za Allaah
ambazo hazipatikani tu katika mwezi huu mtukufu bali
zinapatika siku zote.
7) I'itikaaf
((Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akikaa I'itikaaf kila Ramadhaan katika siku kumi za mwisho, na
mwaka ambao aliondoka duniani alikaa I'itkaaf siku ishirini))
Al- Bukhariy
I'itikaaf ni ibada ambayo
inajumuisha Twa'a nyingi
kama tilawat (kusoma) Qur'aan, Swalah,
Dhikr na Dua'a, na wala haina tabu. Na fadhila zake ni kubwa
mno khaswa katika zile siku kumi za mwisho ndio imo
siku ya Laylatul-Qadr. Ni fursa
kubwa ya mtu kuweza kuupata usiku huo mtukufu kwa kujiepusha
na mambo yanayomshughulisha kila siku ya kidunia na
kuulekeza moyo na nafsi yake katika Twa'a kamili kwa Mola
wake akiwa msikitini.
8) 'Umrah
katika mwezi wa Ramadhaan
Imethibiti katika hadithi kwamba
thawaabu za kwenda 'Umrah katika Ramadhaan ni sawa sawa na
Hija.
((
عمرة في رمضان تعدل حجة )) أخرجه
البخاري و مسلم
(('Umrah katika Ramadhaan ni
sawa (kwa thawabu) na Hija))
Al-Bukhariy na Muslim
9) Baraka
za Suhuur (Daku)
Amesema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
((
تسحروا فإن في السحور بركة )) رواه
البخاري ومسلم
((Kuleni daku kwani katika huko kula daku, kuna baraka))
Al-Bukhariy na Muslim
10)
Du'aa
Ramadhaan ni mwezi wa Du'aa
pia kwani baada ya Allaah
سبحانه وتعالى Kutaja aya za kufunga amendeleza kusema:
}}وَإِذَا
سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ
الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُواْ لِي
وَلْيُؤْمِنُواْ بِي
لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ{{
{{Na waja Wangu watakapokuuliza khabari zangu, waambie kuwa
Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba.
Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate
kuongoka}}.
Al-Baqarah:186
11) Kuomba
Maghfirah na Tawbah
Ramadhaan ni mwezi wa Maghfirah na Tawbah na ni fursa kubwa
kutumia wakati wa Suhuur (kukesha kwa ajili ya kula daku)
kuomba Tawbah na Maghfira kwani Allaah
سبحانه وتعالى ni katika sifa za wenye kupata Pepo.
}}وَبِالأََسْحَارِ
هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ{{
{{Na kabla ya alfajiri
wakiomba maghfira}}
Adh-Dhaariyaat 18
Vile vile Allaah
سبحانه وتعالى Huteremka nyakati hizo katika mbingu
ya kwanza
:
((عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول
الله صلى الله عليه وسلم قال: ينزل ربنا
تبارك وتعالى كل ليلة
إلى
السماء
الدنيا حين يبقى ثلث الليل الآخر
فيقول: من يدعوني فأستجيب له؟ من
يسألني فأعطيه؟
من يستغفرني فأغفر له ))
((Imetoka
kwa Abu Hurayrah
رضي الله عنه
kwamba Mtume
صلى الله عليه وسلم
amesema: Allaah
سبحانه وتعالى
Huteremka kila siku katika mbingu ya dunia (mbingu ya
kwanza) inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na
Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani Ana shida
Nimtekelezee? Nani ananiomba maghfira Nimghufurie? ))
12)
Kuunga udugu na
ujamaa
))
الرحم معلقة بالعرش ، تقول : من وصلني وصله الله ،
ومن
قطعني قطعه الله )) رواه
البخاري ومسلم
((Fuko la uzazi linaning'inia katika 'Arshi linasema,
atakayeniunga Allaah Atamuunga, na atakayenitenga Naye
Allaah Atamtenga [Atamkatia]))
13) Laylatul-Qadr
Ni usiku ambao ibada yake ni
bora kuliko ibada utakayoifanya miezi alfu.
}}إِنَّا
أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ
{{
}}وَمَا
أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ
{{
}}
لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ{{
{{Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri,
Usiku wa Cheo Kitukufu}}
{{Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri}}
{{Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu}}
Al-Qadr
1-3
Basi na tujitahidi ndugu
zetu tusipoteze fursa kubwa ya kuingia katika milango hiyo
mingi ya kheri
ili tutoke katika mwezi huu Allaah
سبحانه وتعالى Akiwa Radhi na sisi na sisi turidhike Naye.
Tutaendelea Inshaa-Allaah Ijumaa ijayo. Tumuombe Allaah
سبحانه وتعالى
Atunufaishe kwa yale tunayojifunza na Atuajaalie miongoni
mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo
njema.
Tunawaombea wote Ijumaa hii iwe ya kheri na baraka nyingi.
Aamiyn
|