">
TAWHIYD
    Tawhiyd

Qur'aan

Sunnah

Fiqhi

Makala

Nasiha Ya Ijumaa

Dua na Adhkaar

'Aqiyda-Tawhiyd

Vitabu

Darsa za Wanawake

    Sikiliza

Qur'aan

Mawaidha

Dua

Nashiyd

    Tizama

Video

 » Mengineyo  

Maana ya Tawbah (Toba)

Maana ya tawbah ni kurudi. Na tawbah inaanza mtu anapoanza kukumbuka madhambi yake, akaingiwa na khofu ya kughadhibikiwa na Mola wake, kisha khofu yake ikampelekea kurudi kwa Allaah سبحانه وتعالى na kumuomba Amsamehe  makosa yake.  

Na tawbah vile vile ni ibada,  haghafiliki nayo mja mwema, hata Mitume ya mwanzo walikuwa wakiomba tawbah.  Kwa hiyo sio khasa kwa wafanyao dhambi tu bali hata kwa waumini, kwani wao pia kuomba tawbah ni sababu ya kufaulu kwao ndio maana Allaah سبحانه وتعالى kasema:  

}} وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ{{

{{Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa}} An-Nuur 31

Baadhi ya watu wanafikiri kuwa tawbah ni kwa sababu ya madhambi makubwa pekee, wakati hakika kila mtu anahitaji kuomba tawbah usiku na mchana kwani madhambi mangapi madogo madogo mtu anayafanya mengine bila ya kujijua  atakuja kuyakuta katika daftari lake ikiwa ataipuuza tawbah. 

Muislam anapofanya maasi ni muhimu kurudi kwa Mola Wake aombe maghfira na tawbah ili airudishe nafsi yake katika kutoharika. Na Allaah سبحانه وتعالى yuko tayari kabisa kupokea tawbah zetu na kutusamehe maovu yetu.

 

}}  وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ{{

{{Naye ndiye anaye pokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa}}  As-Shura 25

Je, nani aliyejidhulumu nafsi yake akawa hana raha na makosa aliyoyafanya? Je, hajui mtu kuwa Allaah ni Mwingi wa Kusamehe na Mwingi wa Rahma? 

 

}}وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللّهَ يَجِدِ اللّهَ غَفُورًا رَّحِيمًا{{

{{Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu}} An-Nisaa 110

Na kama tulivyoona katika aya za nyuma na zifuatazo kuwa Yeye Mwenyewe Ametuamrisha jambo hili :

 

}}وَاسْتَغْفِرُواْ رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُواْ إِلَيْهِ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ{{ 

{{Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu na Mwenye upendo}}Huud 90

 

Na kwa Rahma yake Allaah سبحانه وتعالى hakutuamrisha tu tuombe   tawbah  bali na kutuamrisha pia kukimbilia kuomba hiyo tawbah Kwake

}}وَسَارِعُواْ إِلَى مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ{{

   {Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi}}    

Al-'Imraan 133

 

Lakini mtu anapofanya maasi ni lazima atubie haraka bila ya kusubiri kwani  kuna hatari kubwa ya  kuchelewa kuomba tawbah.