Mahitajio ya miili
yetu (chakula) yote hutoka ardhini ambako ndio
asili ya kuumbwa huu mwili.
الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الأََرْضَ مَهْدًا وَسَلَكَ
لَكُمْ فِيهَا سُبُلاً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاء
مَاء فَأَخْرَجْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّن نَّبَاتٍ
شَتَّى ﴿53﴾ كُلُوا وَارْعَوْا
أَنْعَامَكُمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لأَيَاتٍ
لأُُوْلِي النُّهَى ﴿54﴾ مِنْهَا
خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا
نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَى ﴿55﴾
{{Ambaye
amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na
akakupitishieni humo njia, na akakuteremshieni
kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna
mbali mbali za mimema}}.
{{Kuleni,
na mchunge wanyama wenu. Hakika katika hayo zipo
ishara kwa wenye akili}}.
{{Kutokana
nayo (ardhi) tumekuumbeni, na humo
tunakurudisheni, na kutoka humo tutakutoeni mara
nyengine}}.
Taha: 53 - 55
Nafsi hali
kadhalika mahitajio yake nayo yanotakana na
asili yake ambayo ni kutoka juu kwa Allaah
سبحانه وتعالى
. Kwa hiyo, vitu viwili hivi visipopata
mahitajio yake utaona kuwa vinadhoofika. Mwili
huenda mtu akakonda na kuumwa kwa kutokupata
chakula cha siha, na nafsi ikikosa mahitaji yake
ambayo ni kuwasiliana na kuambatana na Allaah
سبحانه وتعالى
kwa kila aina ya ibada na dhikr, basi nayo
hudhoofika ndio utamuona mtu yuko kwenye maovu
tu, nafsi yake iko mbali na Mola wake, nafsi
nyingine hata haijamtambua Mola wake. Na kwa
mwenye kumjua vile vile kama sisi Waislamu
tunaomuamini Allaah
سبحانه وتعالى,
ikiwa hatuipi nafsi zetu mahitajio yake ndio
utamuoma mtu vile vile yuko kwenye maasi na
mwengine
japo hafanyi
maasi
lakini yuko kwenye dhiki fulani, hana raha kwa
vile ameikosesha nafsi yake mahitajio yake.
Ibada na vitendo vyenye kuambatana na Allaah
سبحانه وتعالى
Jambo la kwanza la kuambatana na Allaah سبحانه وتعالى ni kuitoharisha nafsi kwa kuomba maghfira na kutubu.
Maghfira na toba (tawbah)
Kwa vile binaadamu
sote ni wenye kufanya makosa kila siku
((كل
بني
آدم
خطاء، و خير الخطائين التوابون))
حسن
الألباني
صحيح الجامع
((Kila Binaadamu ni mkosa na mkosa mbora kabisa
ni yule anayeomba toba)). Ameseme Sh Albani ni
Hadithi Hassan kutoka Sahihil-Jaami'i
Kwa Rahma ya
Allaah
سبحانه وتعالى
hata binaadamu awe ana makosa vipi, huenda
akafutiwa dhambi zake zote, kwa hiyo mtu asikate
tamaa au kukhofu kuwa dhambi zake hazitofutwa.
قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى
أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ
إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا
إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿53﴾
{{Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi
zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote.
Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}}
Az-Zumar: 53
Allaah
سبحانه وتعالى
Ametuamrisha tumuombe toba katika aya nyingi za
Qur'aan
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى
اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا ع
{{Enyi
mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo
ya kweli!}}
At-Tahriim 8
وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا
الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
{{Na
tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini,
ili mpate kufanikiwa}}
An-Nuur : 31

