TAWHIYD
    Tawhiyd

Qur'aan

Sunnah

Fiqhi

Makala

Nasiha Ya Ijumaa

Dua na Adhkaar

'Aqiyda-Tawhiyd

Vitabu

Darsa za Wanawake

    Sikiliza

Qur'aan

Mawaidha

Dua

Nashiyd

    Tizama

Video

 » Malezi  

UTANGULIZI

 Suala la malezi ni suala muhimu. Ni suala ambalo kila mmoja wetu amekutana nalo na bado yupo katika kuendelea nalo.Kwa  atakaefanikiwa  ni yule atakaelea watoto wake malezi sahihi ya kiislamu INSHAALLAH.

 

Mlezi anaweza kuwa mzazi halisi (baba na mama) anaweza kuwa mwalimu chuoni au skuli na pia yoyote yule ambao amejikuta katika hali ya kulea ikiwa kama ni mtoto wake au wa mtu mwengine. Ikiwa kila mmoja kati ya hawa atatekeleza jukumu lake vilivyo katika kulea, kuelimisha , kuongoza na kurekebisha ; jamii ya kiislamu nayo ingeliongoka na kuwa ya kupigiwa mfano katika tabia na “akhlaaq” maadili.

 

Na kama moja kati ya viungo hivi muhimu vya malezi vitazembea katika majukumu yake hapo pia kuna hatari kwa jamii ya kiislamu kupotoka kwa kukosa msingi mzuri wa malezi sahihi ya kiislamu .

 

Viungo vyote hivyi vinategemeana . Mzazi/mlezi humtegemea Mwalimu kwani jukumu analolitekeleza Mwalimu na kwa niaba ya mzazi. Na Mwalimu humtegemea mzazi/mlezi kwa kuhakikisha mafundisho anayoyapata mtoto; mzaz/mlezi ana wajibu wa kuhakikisha yanafanyiwa kazi .

 

Lengo kuu la malezi ni katika uislamu ni kumjenga anaelelewa kuwa mfano wa hali ya juu katika jamii. Anatakiwa aandaliwe kujifunga na mola wake, kuwa karibu na mola wake kwa kila jambo analolifanya  . Kuandaliwa kuwa na tabia nzuri ambazo kila muislamu hutakiwa kujipamba nazo kama vile alivyojipamba nazo Mtume wetu (SAW).Kuandaliwa kuweza kuishi katika jamii, kujenga mahusiano mazuri kati yake na wazazi, ndugu na jamaa, rafiki, walimu, majirani na watu wote kwa ujumla . Kuandaliwa vyema mpaka ukifika wakati wa kukabidhiwa majukumu(mukallaf) anakuwa tayari kuyabeba na kuyatekeleza  kikamilifu kwa mujibu wa sheria n.k. Na pia kuandaliwa na kuweza kujua nafasi yake katika maisha mafupi yatakayomkabili na lengo la kuletwa katika ulimwengu huu. Kwa ufupi maandalizi haya yanakuwa katika kiwiliwili, kiakili, kitabia na kiroho.

 

Inshaallahu Taala katika page yetu hii ya malezi tutajaribu kumuomba Allah atupe uwezo wa kujaribu kuwafundisha walezi wetu maadili mema katika malezi, utaratibu  mzuri katika kulea na kutoa “directives” miongozo katika mfumo mzuri wa malezi hasa kwa ndugu zetu wanaoishi nchi hizi za kimagharibi ambao wengi wao kwa bahati mbaya wanapata taabu katika suala zima la malezi kwa sababu ya kuwepo katika nchi ambazo mfumo wao wa malezi upo tofauti kabisa na mfumo wetu. Pia kwa kukosa watu wa kuwaongoza kukabiliana na mtihani huu mzito kwani mara nyingi hujaribu kutafuta ushauri nyumbani(Africa) lakini kwa sababu tayari mazingira ni tofauti ushauri huu unakuwa mara nyingi ni vigumu kutekelezeka.

 

Wabillahi Tawfiq