|
Amesema
Allah (S.W):
Mfano
wa wale
wanaotoa
mali
zao katika
njia ya
Mwenyezi Mungu
ni
kama
mfano wa
punje moja
iliyotoa
mashuke saba,
ikiwa katika
shuke pana
punje mia.
Na Mwenyezi
Mungu huzidisha
amtakaye, (zaidi
kuliko hivi)
na
Mwenyezi Mungu
ni mwenye
wasaa mkubwa
na mwenye
kujua.
Wale
wanaotoa
mali
zao kwa
njia ya
Mwenyezi Mungu,
kisha
hawafuatishi waliyoyatoa-masimbulizi
wala udhia,
wao wana
ujira wao
kwa
Mola wao,
wala haitakuwa
hofu juu
yao
wala
hawatahuzunika. (Al baqarah
2:261, 262)
Na
wanakuuliza
watoe nini?
Sema Vilivyokuzidieni.
(Albaqarah 2:219)
Wanakuuliza
watoe nini?
Sema Mali
yoyote matakayotoa (toeni)
muwape
wazazi, akraba,
mayatima,
masikini na
wasafiri (walioharibikiwa
na waliokuwa
kama
hawa). Na
wema wowote
mnaoufanya
Mwenyezi Mungu
anajua. (Al
baqarah 2: 215)
Enyi
mlioamini!
toeni
katika vile
tulivyokupeni kabla
haijafika siku
amabayo
hapatakuwa kujikomboa
wala urafiki
(wa kusaidiana)
wala uombezi.
Na waliokufuru
ndio
waliojidhulumu (kweli
kweli). (Al
baqarah 2:254)
Enyi
mlioamini!
toeni
katika vile
vizuri mlivyochuma,
na katika
vile tulivyokutoleeni
katika ardhi.
Wala
msikusudie
kutoa vilivyo
vibaya, hali
nyinyi wenyewe
msingevipokea
isipokua kwa
kutoviangalia (basi
Mungu atapokea
kibaya?) basi
jueni kwamba
Mwenyezi Mungu
ni mkwasi
na asifiwaye.
(Al baqarah 2:267)
Wale
watowao
mali
zao usiku
na mchana,
kwa siri
na dhahiri,
wana ujira
wao kwa
Mola wao,
wala haitakuwa
khofu juu
yao
wala
hawatahuzunika.
(Al baqarah 2:274)
Ambao
huamini
yasiyoonekana (maadam
yamesemwa
na
Mwenyezi Mungu
na Mtume
wake na
husimamisha sala
na hutoa
katika yale
tuliyowapa. (Al
baqarah 2:3)
Maamkiano
yao
siku ya
kukutana naye
yatakuwa (ya
salama) na
amani, na
amewaandalia
malipo matukufu. (Al
Ahzab 33:44)
Na
miongoni mwenu
atakayemtii
Mwenyezi Mungu
na
Mtume wake na
kutenda mema.
Tutampa
malipo yake
mara mbili
na kuwaandalia
riziki yenye
hishima. (Al
Ahzab 33:31)
Muamini
Mwenyezi Mungu
na
Mtume wake, na
toeni katika
yale
aliyokupeni. Basi wale
walioamini
miongoni mwenu
na wakatoa,
wana malipo
makubwa. (Al-Hadyad
57:7)
Na
huwalisha chakula
masikini
na
mayatima na
wafungwa, na
hali ya
kuwa wenyewe
wanakipenda (chakula
hicho) (Ad-dahr
76:8)
Soma na
Mola wako
ni karimu
sana
(Alaq 96:3)
Amesema
Mtume Muhammad (S.A.W):
Ogopeni moto
japo kwa
kutoa sadaka
upande wa
tende.
Hakuna
hata siku
moja ambayo
waja
watapambazukiwa ila
malaika wawili
huteremka.
Basi husema
mmoja wao:
Ewe Mola!
mpe
mwenye kutoa
badala yake,
na husema
mwengine: Ewe
Mola! mpe
mwenye kufutika
asiyetoa hilaki
(ya
mali
yake).
Toa ewe
mwanadamu!
utapewa,
sadaka
haipunguzi kitu
katika
mali.
Mtu
mmoja
alimuuliza Mtume (S.A.W): Ni
upi uislam
uliokua bora?
akasema Mtume
(S.A.W), "kulisha
chakula, na
kutoa salamu
kwa unaemjua
na usiemjua."
Mkarimu
yuko karibu
na Allah,
yuko karibu
na pepo,
yuko karibu
na watu.
Mwenye
kumuamini Allah
na siku
ya mwisho
basi amkirimu
mgeni wake.
Amesema
Imam Ally bin
Abi Talib:
Miongoni
mwa amali
bora zaidi
kwa mkarimu
ni kughafilika
na anayo
yajua.
Amesema
Abul-Fathi
Al-bustiy:
Atakaekuwa
mkarimu
kwa ajili
ya
mali,
watu wote
wataelekea
kwake. Na
mali
kwa mwanadamu
ni fitina
kubwa.
Imesemwa:
Hakua
mkarimu anaetoa
baada ya
kuombwa, lakini
mkarimu
ni yule
anaetoa bila
ya kuomba.
Ninaona
watu marafiki
wa ukarimu,
wala sijaona
bakhili katika
ulimwengu kwa
rafiki.
Amesema
Bibi Fatma
(R.A)
Aliye
karibu mno
miongoni mwenu
na Allah
ni aliye
karimu mno
kwenu.
Amesema
Imam Hassan bin Ally bin
Abi Talib:
Atakae
kuwa mkarimu
atapata utukufu,
na atakae
kuwa bakhili
atadharauliwa
na kwa
hakika aliye
mkarimu mno
kwa watu
ni yule
anaetoa na
kumpa
asiyetarajia kitu
kwake na
hakika mkombozi
mkubwa kwa
watu ni
yule
anayekomboa kutokana
na kudra.
Amesema
Jabran Khalily:
Hakuwa
mkarimu
kwa
kunipa mimi
wakati haja
yangu ni
kubwa kuliko
yako, bali
mkarimu ni
kunipa mimi
hali yakuwa
haja yako
ni kubwa
zaidi kuliko
yangu.
Amesema
Goethe
Nipe
na usitaje
na kuzungumza
ulichonipa.
Amesema:
Mchirizi
wa maji
wenye
kumwangilia ni
bora kuliko
mto
usiomwagilia.
Atakaetoa
kwa
ajili ya
mali
aliyokuwa nayo
atapata utukufu
na atakaetoa
kwa ajili
ya kupata
utukufu
atadhalilika.
Aliyemkarimu
mno miongoni
mwa watu
ni
yule anaetoa
kutokana na
kichache
alichonacho na
akauhifadhi uso
wa muombaji
na kudhalilika.
Maneno
ya hekima
ya Waarabu:
Jiepushe
na
uvamizi wa
mkarimu
anapohisi njaa,
mnyonge
anaposhiba.
Methali
za Waaabu:
Mkarimu
anapotoa ahadi
hutekeleza.
Ukarimu
hutokana
na kuwepo.
Methali
za Waswahili:
Mwaka
ni
majira, leo
mvua kesho
jua.
Kutoa
ni
moyo na
wala sio
utajiri
|