Nini maana ya
Qur'aan?
Qur'aan ni maneno ya
Allaah
سبحانه وتعالى
yaliyoletwa kama 'Wahyi' (Ufunuo)
kwa Mjumbe wa Allaah
سبحانه وتعالى
na Mtume wa mwisho
Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم
, yaliyoandikwa
katika Misahafu, yanayorithiwa na vizazi kwa vizazi,
yaliyonukuliwa kwa
mapokezi mengi, kusoma kwake ni ibaada, ni yenye miujiza
hata kama ni sura ndogo kabisa, na ni uongofu kamili wa watu
wote. Kama Asemavyo Allaah
سبحانه وتعالى:
}}الَر
كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ
الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ
الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ{{
{{Alif Lam Ra.
(A.L.R.) Hichi ni Kitabu Tulicho kiteremsha kwako ili
uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye muwangaza, kwa
idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye
nguvu, Msifiwa}}
Ibraahiym:1
Majina ya Qur'aan
Ma'ulamaa na Wafasiri wa
Qur'aan wametaja majina mengi ya Qur'aan kutokana na
dalili katika Qur'aan yenyewe na
pia Hadiythi Sharifu. Yafuatayo ni baadhi ya majina hayo:
1) Kitabu
}}ذَلِكَ
الْكِتَابُ لاَ رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ{{
{{Hiki ni
Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uongofu kwa
wachamungu}}
Al-Baqarah:2
2)
Al-Furqaan (Upambanuzi)
}}تَبَارَكَ
الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَى عَبْدِهِ لِيَكُونَ
لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا{{
{{Ametukuka
Aliyeteremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa
walimwengu wote}}
Al-Furqaan: 1
3) Adhikr
(Ukumbusho)
}}وَهَذَا
ذِكْرٌ مُّبَارَكٌ أَنزَلْنَاهُ أَفَأَنتُمْ لَهُ مُنكِرُونَ{{
{{Na haya ni
makumbusho yaliyobarikiwa, Tuliyoyateremsha. Basi je!
Mnayakataa?Al
Anbiyaa:50
4) An-Nuur
(Mwangaza)
}}يَا
أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ
وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا{{
{{Enyi watu!
Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na
Tumekuteremshieni Nuru iliyo wazi}}
An-Nisaa 174
5) Mawaidha
}}يَا
أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ
وَشِفَاء لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ{{
{{Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu
Mlezi, na poza kuponyesha yaliyomo vifuani, na uongofu, na
rehema kwa
Waumini}} Yuunus:57
Bila ya
shaka Qur'aan ni kitabu kitukufu kabisa anachokihitajia kila
mtu kumpatia uongofu kamili awe katika njia iliyonyooka na
awe katika Twa'a ya Mola Wake Mtukufu. Naye Allaah سبحانه
وتعالى
Ametuhakikishia kuhifadhiwa na kuthibitika kwake ili
isiongezeke au kupungua hata neno au herufi moja ikaja ikawa
hii Qur'aan imechanganyika na maneno ya mtu bali, ibakie
kuwa ni maneno Yake Pekee Mola wa viumbe vyote.
Amesema
Allaah
سبحانه وتعالى
}}إِنَّا
نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ{{
{{Hakika Sisi
ndio Tulioteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio
Tutaokaoulinda}}
Al-Hijr: 9
}}إِنَّ
الَّذِينَ كَفَرُوا بِالذِّكْرِ لَمَّا جَاءهُمْ وَإِنَّهُ
لَكِتَابٌ عَزِيزٌ{{
}}لاَ
يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ
تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ{{
{{Kwa hakika
wanayoyakataa mawaidha haya yanapowajia (wataangamia), na
haya bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu}}
{{Hautakifikia
upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye
hikima, Msifiwa}}
Fusswilat:41-42
Kuteremshwa
Qur'aan katika Ramadhaan.
Anasema
Allaah
سبحانه وتعالى
}}شَهْرُ
رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ
وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ{{
{{Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur'aan kuwa ni
uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na
upambanuzi}}
Al-Baqarah: 185
Qur'an imeteremshwa kwa
miteremsho ya aina mbili kama ifuatavyo:
1)
Mteremsho wa
mara moja
Imeteremshwa Qur'aan kamili kutoka 'Lawhi-m-Mahfuudh' (Ubao
uliohifadhiwa) mpaka mbingu ya kwanza. Kama
inavyothibitishwa na kauli
ya Allaah
سبحانه وتعالى :
}}إِنَّا
أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْر{{ِ
{{Hakika Sisi
Tumeiteremsha Qur'aan katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo
Kitukufu}}
Al-Qadar: 1
}} إِنَّا
أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ إِنَّا كُنَّا
مُنذِرِينَ{{
{{Hakika
Tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni
Waonyaji}}
Ad-Dukhaan: 3
2) Mteremsho
wa kidogo kidogo
Imeteremshwa kwa muda wa miaka 23 tokea kupewa utume Mtume
Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم
hadi kufa kwake, nayo
imeteremshwa kidogo kidogo kutokana na hali na matukio
yaliyokuwa yakitokea.
Aya za mwanzo kuteremshwa
ni Aya tano katika Surat Al-'Alaq
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
}}اقْرَأْ
بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ
{{
}}
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ{{
}}
اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ{{
}}
الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ
{{
}}عَلَّمَ
الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ
{{
KWA JINA LA
MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
{{Soma kwa
jina la Mola wako Mlezi Aliyeumba}}{{Amemuumba binaadamu kwa
tone la damu}}
{{Soma! Na
Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!}}{{Ambaye
Amefundisha kwa kalamu}}
{{Kamfundisha
mtu aliyokuwa hayajui}}
Al-'Alaq:1-5
Kutokana na rai zilizo za
nguvu kabisa na zilizowafikiana zaidi, kwamba Aya ya mwisho
kuteremshwa ni,
}}وَاتَّقُوا
يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ
إِلَى اللَّهِ ثُمَّ تُوَفَّى كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ
وَهُمْ لا يُظْلَمُونَ{{
{{Na iogopeni
Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi
italipwa ilichochuma.
Nao hawatadhulumiwa}}
Al-Baqarah:281
Vipi ilikuwa
ikiteremshwa Qur'aan?
Kuteremeshwa Qur'aan katika kifua chaMtume
صلى الله عليه وآله وسلم
ilikuwa ni kutokana na 'Wahyi'
(ufunuo) kama ilivyothibiti katika Qur'aan yenyewe.
}}وَكَذَلِكَ
أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّتُنذِرَ أُمَّ
الْقُرَى وَمَنْ حَوْلَهَا{{
{{Na namna
hivi Tumekufunulia Qur'aan kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa
Mama wa Miji na walio pembezoni mwake}}
Ash-Shuura:7
}}نَحْنُ
نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا
أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن
قَبْلِهِ لَمِنَ
الْغَافِلِينَ{{
{{Sisi
Tunasimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur'aan hii. Na
ijapokuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa wasiojua}}Yuusuf:3
}}اُتْلُ
مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ{{
{{Soma
uliyofunuliwa katika Kitabu}}
Al-'Anqabuut: 45
Kwa
nini imeteremshwa kidogo kidogo na sio
uteremsho mmoja
kamili?
Makafiri
waliteta kuhusu Qur'aan kama ilivyo kawaida yao na ukaidi
wao wa kukanusha kwa kila aina ya vitimbi na usemi,
wakasema:
}}وَقَالَ
الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ الْقُرْآنُ
جُمْلَةً وَاحِدَة{{
{{Na wakasema
waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur'aan kwa jumla
moja?}}Al-Furqaan:32
Wakikusudia kwa nini
haikuteremshwa Qur'aan kama vitabu vya nyuma navyo ni
Tawraah, Injiyl, Zabuur na kadhalika
ambavyo viliteremshwa kwa jumla moja?
Allaah
سبحانه وتعالى
Akawajibu kwa kuwapa Hikma Yake ya kuiteremsha kidogo kidogo
kwa muda wa miaka ishirini na tatu kutokana na matukio na
hali ilivyokuwa ikitokea, kuwa
ili Qur'aan ithibitike katika moyo wa Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
kama aya ilivyomalizikia kusema.
}}وَقَالَ
الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ الْقُرْآنُ
جُمْلَةً وَاحِدَة كَذَلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِ فُؤَادَكَ
وَرَتَّلْنَاهُ تَرْتِيلًا
{{
{{Na wakasema
waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur'aan kwa jumla moja?
Hayo ni hivyo ili tuuthibitishe moyo wako, na ndio tumeisoma
kwa mafungu }} Al-Furqaan: 32
Vile vile
Amesema Allaah
سبحانه وتعالى :
}}وَقُرْآناً
فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَى مُكْثٍ
وَنَزَّلْنَاهُ تَنزِيلاً{{
{{Na Qur'aan
Tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo,
na Tumeiteremsha kidogo kidogo}}Al-Israa:106
Tutaendelea Inshaa-Allaah Ijumaa
ijayo. Tumuombe Allaah
سبحانه وتعالى
Atunufaishe kwa yale tunayojifunza na Atuajaalie ni miongoni
mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo
njema.
Tunawaombea wote
Ijumaa hii iwe ya kheri na baraka nyingi. Aamiyn