|
((عن
عائشة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم " كان إذا
دخل العشر أحيا الليل وأيقظ أهله وشد مئزره ))
البخاري
ومسلم زاد مسلم وجَدَّ وشد مئزره .
((Bibi 'Aishah
رضي الله عنها
amesema
"Zilipokuwa zikiingia siku kumi za mwisho (za Ramadhaan),
Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa
akiuhuisha
usiku kwa kufanya ibada, akiamsha aila (familia) yake usiku,
na akikaza Izaar yake (shuka inayovaliwa kiunoni kwa maana
kuwa alikuwa akijibidiisha sana)
[
Al-Bukhaariy na Muslim]
Muslim akazidisha, akijitahidi na akikaza Izaar yake
Hadiyth hii ni
uthibitisho
kuwa siku kumi za mwisho za Ramadhaan zina fadhila khaswa na
kubwa kuliko siku zozote nyingine ambazo Muislamu inampasa
aongeze twa'aa na vitendo
vya ibada
kama
kuswali, kufanya dhikir (kumkumbuka Allaah
سبحانه وتعالى
kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr) na kusoma Qur'aan.
Bibi 'Aishah
رضي الله عنها
ametuelezea kuhusu Mtume wetu
صلى الله عليه وآله وسلم
kama mfano bora kabisa kwa sifa nne zifuatazo:
1) Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa "akiuhuisha (akikesha usiku)
katika ibada"
Ina maana kwamba, alikuwa halali usiku. Kwa hiyo yeye Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa akikesha usiku mzima kufanya ibada na akiifufua
nafsi yake kwa kutumia usiku wake kukaa macho
na kuacha
kulala. Hii ni kwa vile kulala usingizi ni mauti madogo.
Maana ya "akihuisha (akikesha usiku)"
ni kwamba yeye Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa akitumia wakati huo katika hali ya qiyaam (kusimama
kuswali usiku) na kufanya vitendo vya ibada ambavyo
vinafanywa kwa ajili ya Allaah
سبحانه وتعالى
Mola wa Ulimwengu. Inatupasa tukumbuke siku kumi za mwisho
za Ramadhaan ni chache zilizokadariwa kwa nambari.
Ama kuhusu
ilivyoripotiwa katika Hadiyth ya 'Abdullah ibn 'Amr kwamba
imekatazwa kukesha usiku mzima katika Swalah, hii inahusu
mtu anayefanya hivyo kwa mfululizo wa siku zote za mwaka.
2) Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa "akiamsha 'aila (familia) yake"
Ina maana kwamba ni wake zake
صلى الله عليه وآله وسلمwaliotwaharika,
Mama wa Waumini, ili nao wanufaike katika ibada njema hizo
za dhikr
(kumkumbuka Allaah)
na vitendo vyote vingine vya ibada katika siku hizo zenye
baraka nyingi.
3) Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa "akifanya bidii"
Ina maana kwamba yeye Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa akijizuia
na akijitahidi
sana katika ibada, akiongeza vitendo vyema zaidi kuliko
alivyokuwa akifanya siku ishirini za mwanzo (wa Ramadhaan).
Akifanya hivi kwa sababu Laylatul-Qadr inatokea katika usiku
mmoja wa siku hizo kumi.
4) Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
"akikaza izaar (shuka) yake"
Ina maana kwamba,
akijikaza na kufanya bidii kubwa katika jitihada ya
kufanya ibada
nzito. Inasemekeana vile vile kuwa Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa akijitenga na wake zake. Hii ni rai iliyo sahihi
kabisa kwa vile
inakubaliana na ilivyotajwa kabla
katika Hadiyth ya Anas
رضي الله عنه
"Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa akikunja kitanda chake
na
akijitenga na wanawake (yaani wake zake)"
[ Tazama Lataa'if-ul-Ma'aarif, Ukurasa 219]
Vile vile Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
alikuwa akifanya I'tikaaf katika siku za mwisho za Ramadhaan
na watu wenye kuwa katika hali ya I'itikaaf
hujizuia
na jimai (tendo la ndoa) na wake zao.
Kwa hiyo
enyi ndugu Waislamu, jitahidini
kujizoesha
na kuwa katika sifa na khulka
hizi. Na chungeni Swalah za usiku (Tahajjud) pamoja na Imaam
hata baada ya kuswali Tarawiyh (ambayo inaswaliwa katika
nyakati za mwanzo za usiku) ili jitihada zenu katika siku
hizi za kumi za mwisho zipindukie siku ishirini za mwanzo na
ili mpate kufaulu kupata sifa ya "kuuhuisha
usiku
kwa ibada" kwa kuswali.
Na ni lazima muwe na subira katika twa'a ya Allaah
سبحانه وتعالى
na ibada za usiku kwani hakika Tahajjud (Swalah ya usiku)
ni ngumu lakini thawabu zake ni kubwa sana. Naapa kwa
Mwenyeezi Mungu, ni fursa kubwa katika maisha ya Muislamu na
vile vile ni faida kubwa kuitumia fursa hii kwa yule
aliyejaaliwa kupewa na Allaah
سبحانه وتعالى (kuwa
hai na uzima). Kwani binaadamu hawezi kujua kama ataweza
kuchuma tena thawabu nyingi kama hizi, ambazo zitamfaa
katika maisha yake ya dunia na ya Akhera.
Salaf
Swaalih (Wema waliotangulia) wa Ummah huu walikuwa
wakijitahidi katika ibada za siku hizi kwa kuzirefusha
Swalah za usiku. As-Swaa'ib bin Yaziyd amesema, "'Umar bin
Al-Khatwaab alimuamrisha 'Ubay bin Ka'ab na Tamiym Ad-Daariy
kuimamisha (kuongoza) watu katika Swalah kwa Raka'ah kumi na
moja. Imaam alikuwa akisoma aya mia moja hadi ilibidi
tuegemee mkongojo kwa sababu ya
kisimamo kirefu, na
tulikuwa hatupumziki hadi inapoanza kuingia Alfajiri".
[Tazama Al-Muwattwa, Mjalada 1, Ukurasa 154]
'Abdulllah
bin Abu Bakkar amesema "Nimemsikia baba yangu (Abu Bakkar)
akisema, wakati wa Ramadhaan, tulikuwa tukichelewa kumaliza
Swalah za usiku (hadi karibu na Alfajiri) hata tukiwahimiza
watumishi kutuwekea suhuur (daku) kwa kuogopa Alfajiri
isitufikie"
[Muwatta
ya
Imaam Maalik, Mjalada 1, Ukurasa156]
Nafsi ya muumini inapambana na jitihada mbili katika
Ramadhaan; Jitihada ya mchana
kwa
kufunga na jitihada ya usiku kwa Qiyaam (Swalah ya kusimama
usiku). Kwa hiyo yeyote atakayejumuisha jitihada mbili hizi
na akatimiza haki zake,
basi yeye atakuwa miongoni mwa wenye subira
kama
Alivyosema Allaah
سبحانه وتعالى
((إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم
بِغَيْرِ حِسَابٍ))
((Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu))
[Az-Zumar:10]
Siku kumi hizi ni za mwisho
katika mwezi mtukufu huu na vitendo vya Muislamu
vinahesabika zaidi vile vya mwisho. Kwani huenda akafaulu
kukutana na usiku wa Laylatul-Qadr wakati
akiwa amesimama katika Swalah ikawa ni fursa nzuri ya
kufutiwa madhambi yake yote na
Allaah
سبحانه وتعالى.
Ni wajibu wa kila mtu kuamsha, kushawishi, kuhimiza na
kushurutisha 'aila (familia) yake kutenda vitendo vya ibada
khaswa katika nyakati hizi tukufu, kwani hakuna
atakayedharau kufanya hivi ila yule aliyenyimwa fadhila hizi.
Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba wakati wengine wako
katika ibada khaswa za
masiku haya kumi, wengine
wanatumia wakati wao katika vikao vya
maasi. Hakika hii ni
khasara kubwa. Tunamuomba Allaah
سبحانه وتعالى
Atuhifadhi na Atuhidi.
Kwa hiyo
Muislamu atakayejishughulisha na kutenda vitendo vyema na
ibada katika siku kumi hizi za mwisho atakuwa amejiingiza
katika milango ya kuchuma mema yaliyobakia katika mwezi huu
mtukufu. Ni khasara kwa mtu aliyeanza mwezi wa Ramadhaan kwa
kusimama kwa nguvu kuswali, kusoma Qur'aan na dhikir, kisha
siku za mwisho akawa
na
'ajzi (akawa mzito na mvivu)
katika kufanya ibada, wakati hizi siku za mwisho ndio siku
zilizokuwa muhimu na zenye uzito wa thawabu ya kusimama
kuswali na mengineyo kuliko
zote. Hivyo kila mmoja inampasa aongeze bidii zaidi na
kujitahidi kwa kadiri awezavyo
kuongeza vitendo vyema na ibada katika kumalizia mwezi
mtukufu huu. Na kukumbuka kuwa amali za mtu zinahesabika
zile za mwisho.
DU'AA YA
LAYLATUL-QADR
Katika siku
hizi kumi za mwisho ni vizuri sana kuisoma Du'aa hii kila
mara khaswa katika usiku wa Laylatul-Qadr kama
ilivyothibiti katika
Hadiyth ifuatayo:
(عن عائشة رضي الله عنها أنها قالت يا رسول
الله أرأيت إن وافقت ليلة القدر
ما أدعو قال تقولين اللهم
إنك عفو تحب العفو فاعف عني)) ابن
ماجه و صححه الألباني
((Kutoka kwa Bibi 'Aishah
رضي الله عنها
kwamba
alisema "Ewe Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
je, nitakaposimama usiku wa Laylatul-Qadr niombe nini?"
Akasema, "Sema Ee Mwenyeezi Mungu Hakika Wewe Ndiye Mwenye
Kusamehe Unapenda Kusamehe basi Nisamehe"))
[Ibn Maajah na kaisahihisha
Albaniy]
MATAMSHI
YAKE
Allaahumma
Innaka 'Afuwwun Tuhibbul-'Afwa Fa'afu 'Anniy
|