|
|
|
|
 |
|
» Makala na
Mengineyo |
 |
|
 |
|
Suluhisho La Matatizo Ya Umma Huu
Na: Imaam Muhammad Naasir ud-Deen al-Albaanee
Asili: Manhaj ya Salafi
Imefasiriwa Na: Abufarida Muhammad A. Basawad |
Mwanachuoni mkubwa wa hadhith wa karne hii (ya ishirini), Sheikh
Muhammad Naasir ud-Deen al-Albaani (rahimahullah) aliulizwa: "Ni kwa
misingi ipi, ulimwengu wa leo wa ki-islamu unaweza ukaregeshwa
katika hali yake ya upya?"
Nae akajibu: "Mimi naamini yakwamba riwaya zilizopokewa katika
hadith zilizo sahih zinabainisha jawabu waziwazi kwa maswali kama
hayo na mfano wake ambayo yaliyo kithiri kwenye zama zetu hizi. Nao
ni msemo wake (S.A.W): 'Mutakapo jishughulisha na biashara za riba
na kushikamana na mikiya ya ng'ombe, na mukaridhika na mambo ya
ukulima (mashamba) na mukawachana na kupigana jihaad kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu (Swt), basi Mwenyezi Mungu atawadhalilisha. Na
hatowaondolea udhalilifu huo mpaka muregee kwenye dini yenu'".1
Kwahivyo kurudi katika dini, ndio msingi mkubwa . Hali hii pia
imezungumzwa na Imam Maalik (rahimahullah) katika msemo wake
unaostahiki kuhifadhiwa kwa wino wa dhahabu .Nae Amesema:"Yeyote
aneanzisha katika Uislamu jambo la uzushi ,na akalidhania kuwa ni
zuri ,basi huyo amedai yakwamba Mtume Muhammad(S.A.W) amefanya
khiyana katika (amana ya kuufikiliza) ujumbe. Soma maneno ya
Mwenyezi Mungu, Alietukuka na Mwenye Nguvu: "Leo nimekukamilishieni
dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na nimekupendeleeni Uislamu
uwe dini yenu."2
Kwahivyo, chochote ambacho hakikuwa (katika sehemu ya )dini siku
hiyo, si (katika sehemu ya) dini leo hii. Na sehemu ya mwisho ya
Umma huu hautorekebishika, isipokuwa kwa kile kilichourekebisha
sehemu yake (umma huu) yakwanza.
Kwahivyo, kama ilivyokuwa hali ya waarabu wakati wa siku za ujinga (jaahilyya)
haikurekebishwa mpaka alipokuja Mtume (S.A.W) na risala kutoka
mbinguni (wahyi) ndipo wao walipoupata uongofu hapa duniani, ambao
ndio utakaowaokoa kesho (Aakhera). Kuimarisha misingi ya hali njema
ya Uislamu ulio bora kwenye zama zetu hizi, si jengine isipokuwa ni
kuregea kwenye Qur'aan na Sunna.
Ingawaje, jambo hili lahitaji kutiliwa mkazo katika kulidhihirisha,
kutokana na idadi kubwa ya mapote ya ki-islamu na vyama
vilovyojitokeza kwenye majukwaa wakidai kuwa wapo juu ya njia ambayo
jamii ya ki-islamu na utawala wa ki-islamu unaweza ukaanzishwa.
Tunajua sisi kutoka kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za
Mtume Wake (S.A.W) yakwamba njia ya kuelekea katika kulitekeleza (lengo)
hili ni moja tu, nalo ni lile ambalo Mwenyezi Mungu (Swt) Alolitaja
pindi Aliposema: "Na kwa hakika hii ndio njia yangu iliyonyoka.Basi
ifuateni wala msifuate njia nyengine, zikakutengeni mbali na njia
Yake (Mwenyezi Mungu)"3.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akawafafanulia maswahaba zake. Siku
moja aliwachorea mstari ulionyoka kwenye ardhi na kisha akachora
vistari vyengine vidogo pambizoni mwake. Kisha, muda ule-ule
kilipokuwa kidole chake kitukufu kikisongea juu na chini ya ule
mstari ulionyoka, aliisoma hiyo aya iliyopita . Kisha akawaonyesha
vile vistari vidogo alivyochora mule pambizoni mwa ule mstari
ulionyoka na akasema: "Hii ni njia ya Mwenyezi Mungu na hizi ni njia
(nyengine).Katika kila kilele cha hizi njia (nyengine),kuna shetani
anae-itisha watu kuelekea kwenye mwito huo."4
Juu ya hayo, Mwenyezi Mungu (Swt) ayakinisha kwenye aya nyengine,
kama alivyosema katika aya iliyopita pamoja na maelezo ya Mtume (S.A.W)
kama ilivyoelezwa kwenye hadith. Kwahivyo Akasema Mwenyezi Mungu (Swt):"Na
atakaemwasi mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na akafuata njia
isiyokuwa ya waumini tutamgeuza alikogeukia mwenyewe na tutamwingiza
katika jahannam ;napo ni pahali pabaya kabisa pa mtu kurudia."5
Katika aya hii kuna hikma kubwa iliyofichamana, kwani Mwenyezi Mungu
(Swt) , Aliekamilika, Amezifungamanisha "njia za waumini" na
aliyokuja nayo Mtume(S.A.W). Vile-vile Mtume (S.A.W)akatuashiria
nukta hii katika hadith kuhusu kugawanyika kwa umma na kuwa mapote.
Kwahivyo, alipoulizwa kuhusu pote litakalo okoka, akajibu kwa kusema:
"Ni lile ambalo (liloshikamana kwa yale) nilojitegemeza nayo mimi na
maswahaba zangu leo." 6
Pana hikma gani pale Mwenyezi Mungu (Swt) kutaja "njia ya waumini"
kwenye aya hii? Na pana maana gani kwa Mtume (S.A.W) kujiunganisha
yeye na maswahaba zake kwenye hiyo hadith iliyopita?
Jawabu ni kwamba: Hawa maswahaba watukufu ndiwo waliozipokea hizo
risala mbili (Qur'an na Sunna) kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W),
na kupewa ufafanuzi wake na yeye Mtume (S.A.W) moja kwa moja, pasi
na kuwepo mjumbe yeyote. Lakini, ilikuwaje hali ya walokuja baada
yao? Hapana shaka yakwamba hali hii ni kama alivyosema Mtume (S.A.W):
"Hakika, yule aliyeko huona jambo lisilo-onekana na asokuweko."7
Hii ndiyo sababu Imani (kuamini) ya Maswahaba wa kwanza ilikuwa
thabiti zaidi kuliko ya wale walokuja baada yao. Na hivi ndivyo
alivyotueleza mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) katika hadithi
mutawaatir: "Bora ya watu ni karne yangu, kisha ni wale walokuja
baada yao na kisha ni wale walokuja baada yao."8
Kulingana na hadithi hii Muislamu hafai kujitegemea yeye mwenyewe
binafsi katika kuifahamu Qur'an na Sunna. Ni afadhali atafute
usaidizi katika kuvifahamu vitu viwili hivyo kwa kutaraji msaada wa
maswahaba watukufu, kwani ni wao walokuwa wapokezi wa Mtume (S.A.W),
na wakafahamishwa wakati mwengine kwa kutamka, na wakati mwengine
kwa vitendo na kwa wakati mwengine kuwaruhusu kwa kuwanyamazia.
| |
 |
|
|
 |
|
|
| |
|
|
|
|
|
|
 |
 |
|
|
|