">
TAWHIYD
    Tawhiyd

Qur'aan

Sunnah

Fiqhi

Makala

Nasiha Ya Ijumaa

Dua na Adhkaar

'Aqiyda-Tawhiyd

Vitabu

Darsa za Wanawake

    Sikiliza

Qur'aan

Mawaidha

Dua

Nashiyd

    Tizama

Video

 » Mengineyo  

Vipi Kuomba Maghfira Na Tawbah?

Ikiwa Mtume صلى الله عليه وسلم  ambaye amefutiwa madhambi  yake yaliyotangulia na yajayo na alikuwa akiomba kila siku maghfira na tawbah kwa Allaah سبحانه وتعالى , seuze sisi?

Kwa hiyo inampasa Muislamu kila siku aombe maghfria na tawbah mara mia au zaidi kwa siku kama alivyokuwa akifanya Mtume صلى الله عليه وسلم kama tunavyona katika hadithi hii:

((عن أبي هريرة رضي الله عنه، قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:   والله إني لأستغفر الله وأتوب إليه في اليوم أكثر من سبعين مرة))   رواه البخاري .

 (( Imetoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه alimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم  akisema: Wallahi mimi naomba maghfira kwa Allaah na kutubu Kwake zaidi ya mara sabiini kwa siku )) Imesimuliwa na Al-Bukhari

  وفي حديث آخر عند مسلم قال:  يا أيها الناس توبوا إلى الله  واستغفروه فإني أتوب في اليوم مائة مرة))

 Katika hadithi nyingine kutoka kwa Muslim kasema:  Enyi Watu tubuni kwa Allaah na muombe magfhira kwani mimi huomba tawbah mara mia kwa siku))

 

Rakaa  mbili za  Swalaatu-tawabah                                                                                            


 

 )ما من رجل يذنب ذنبا، ثم يقوم فيتطهر، ثم يصلي، ثم يستغفر الله، إلا غفر الله له، ثم قرأ هذه الآية }}والذين إذا فعلوا فاحشة أو ظلموا أنفسهم ذكروا الله{{ ، إلى آخر الآية((   رواه ابو داود و الترمذى و النسائي عن أبي بكر الصديق رضى الله عنه صحيح الألباني صحيح الترغيب  


 

 

((Yeyote atakayefanya dhambi kisha akachukua wudhuu, kisha akaswali, kisha akaomba maghfira basi Allaah سبحانه وتعالى Atamghufuria, kisha akasoma ayah hii: {{Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu}}  mpaka mwisho wa aya))  Imepokelewa na Abu Dawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasaai, na Abu Bakr رضى الله عنه  - Imesahihishwa na Sh.Albani.

Bwana Wa istighfaar

 

((وعن شداد بن أوس رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال:   سيد الاستغفار أن يقول العبد :    

 

((اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك ، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت ، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت ، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ  عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ)) . رواه البخاري في صحيحه

Imetoka kwa Shaddaad Bin 'Aws  رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم  kasema, Bwana wa Istighfaar  ni kusema:

“Ewe Mwenyezi Mungu  Wewe ni Mola wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja wako, nami niko juu ya  ahadi yako, na agano lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda kwako kutokana  na shari ya nilichokifanya, nakiri  kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehi madhambi ila Wewe)) Al-Bukhaari

 

Dua ya Nabii Yunus Alayhis-salaam alipokuwa tumboni mwa  samaki

 

}}لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ{{

{{Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu}} Anbiyaa 87

 

Tasbihi zenye kufuta dhambi

 

((قال النبي صلى الله عليه وسلم :   من قال سبحان الله وبحمده في يوم مائة مرة غفرت له ذنوبه وإن كانت مثل زبد البحر))

((Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم  ‘Mwenye kusema   سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ “Ametakasika Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote ni zake"  kwa siku mara mia, atafutiwa madhambi yake hata kama yalikuwa mfano wa povu la bahari
 

 

((قال صلى الله عليه وسلم من قال حين يأوي إلى فراشه :  لا إله إلا الله وحده لا شريك له،له الملك،وله الحمد،وهو على كل شيء قدير، لاحول ولا قوة إلا بالله العلى العظيم،سبحان الله، والحمد لله،ولا إله إلا الله،والله أكبر ؛غفرت له ذنوبه أوخطاياه    وإن كانت مثل زبد البحر))   صحيح الألباني صحيح الترغيب  

 

 

((Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم  anapokwenda mtu kulala kitandani mwake akasema :

لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك،وله الحمد، وهو على كل شيء قدير، لاحول ولا قوة إلا بالله العلى العظيم،سبحان الله،والحمد لله،ولا إله إلا الله،والله أكبر

 

 

Hufutiwa dhambi zake hata kama zilikuwa mfano wa povu la bahari))  Imetoka katika Sahiih Targhiib   Kaisahihisha Sheikh Albaani