|
|
|
|
 |
|
» Makala na
Mengineyo |
 |
|
 |
Wajibu Wa Kushikamana na Jama'aah
Imetayarishwa Na: Shaikh Abdus Salaam Ibn
Burjiss
Asili: Al-Amr Bi-Luzoom Jama'at-il-muslimeen. (tazama
SSNA)
Imefasiriwa Na: Abu Malaadh Said bin Baadel al-Hadhramee |
Kuna maafikiano makubwa baina ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa'ah kuwa
ni wajibu wetu kushikamana na Jamaa'ah na kuwa imekatazwa kujitenga
nayo; Kushikamana na Jamaa'ah ni jambo jema na kujiepusha na
kujitenga nayo ni ufisadi.
Kuna dalili nyingi kutoka katika Qur'aan na Sunnah ambayo imetaja
kuhusu jambo hili, mpaka kufikilia kiwango cha kuwa tawaatur. Vile
vile kuna riwaya chungu nzima kutoka kwa ma salaf (watangulizi wetu
wema) kuhusiana na haya. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'aalah)
Akasema: "Na mushikamane na Kamba ya Mwenyezi Mungu, nyote kwa
pamoja, wale musifarikiane" (Surat- Aal-Imraan 3:103)
Ibn Abee Haatim[2] amesema: "Babangu alinieleza kuwa: Amr Ibn 'Alee
As-Sairafee alinieleza, akisema: Abdu Rabbihi Ibn Baariq al-Hanafee
- na akamsifu kwa uzuri - kuwa alinihadithia na kusema: Simaak Ibn
al-Waleed al-Hanafee amesema yakuwa alikutana na Ibn 'Abbaas mjini
al-Madinah na akamwambia:"Wasemaje kuhusu huyu kiongozi wetu
anayetutawala, na kutunyanyasa (kutudhulumu na kutukandamiza) na
kutushtumu, jee ni kwa nini basi tusimzuie (yaani tumpige vita na
kumpinga)?"
Ibn Abbas akamjibu:"Laa! bali mumtii, Ewe Hanafee". Na akaendelea
kusema: "Ewe Hanafee, (shikamana na ) Jamaa'ah, Jamaa'ah! Kwa hakika
mataifa yalio watangulia waliangamizwa kwa ajili ya kujigawanya (kufarikiana
wao kwa wao). Jee hukusikia Mwenyezi Mungu aliposema: "Na
mushikamane na Kamba ya Mwenyezi Mungu, nyote kwa pamoja, wala
musifarikiane...."
Amesema Ibn 'Atiyyah katika tafseer yake [3], "Rai za wanavyuoni wa
tafseer zimetofautiana kuhusu maana ya hii sehemu ya ayah "Kamba ya
Mwenyezi Mungu". Basi Ibn Mas'ood akasema "Kamba ya Mwenyezi Mungu (ina
maanisha) ni Jamaa'ah". Anas Ibn Malik anatueleza kuwa mtume wa
Mwenyezi Mungu (Salallahu 'alayhi wasallam) amesema: "Kwa hakika
banu Israeel waligawanyika mapote sabiini na moja . Ummah wangu
utagawanyika mapote sabiini na mbili - yote hayo ni yenye kuangamia
katika (moto wa) Jahannam isipokuwa moja. (Maswahaba)
wakamuuliza:"Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni kundi gani litakalo
okoka?" Naye akakunja ngumi na kusema;"Jamaa'ah", halafu akawasomea
aya "Na mushikamane na Kamba ya Mwenyezi Mungu, nyote kwa pamoja"
[4].
Ibn Mas'ood alisema katika moja ya khutbah zake:"Nyinyi nyote kwa
ujumla, munawajibika kuwa watiifu (kwa Allah) pamoja na Jamaa'ah,
kwani hii ndiyo Kamba ya Allah aliotuamrisha sisi Mola wetu."
Qataada naye akasema:"Kamba ya Allah ambayo Ametuamrisha tushikamane
nayo ni Qur'aan". Nae As-Suddee akasema: "Maana ya Kamba ya Allah ni
kitabu chake Mwenyezi Mungu". Ibn Mas'ood na Ad-Dahhaak pia walisema
hivyo. Na mengine mengi pia yalisemwa ambayo yamefanana na haya (katika
misemo iliotangulia).
Neno "jamee'an" (nyote kwa pamoja) imeungana na amri " 'I'tasimoo" (shikamaneni),
basi maana yake itakuwa "muwe wamoja juu ya kushikamana na hiyo
Kamba ya Allah". Na "musifarikiane" ina lenga aina ya migawanyo
ambayo haitawafanya mushiriki katika Jihaad na mambo ya kulinda dini
na Neno la Mwenyezi Mungu. Huu ndiwo mgawanyiko uliotokamana na
fitna na kutokubaliana katika mambo ya imani." [mwisho wa maneno ya
Ibn 'Atiyyah]
Nami nasema kuwa, kutofautiana katika tafseer ya "Kamba ya Allah" ni
tofauti inayo tuashiria aina nyingi ya maana ya neno hilo, wala sio
tofauti ya maana halisi ya neno hilo, kama tulivyoelezwa na Ibn
'Atiyyah, Ibn 'Abdil-Barr na muhaqqiqeen wengineo. Na maoni yake
kuwa (Kamba ya Mwenyezi Mungu) inamaanisha Kitabu chake inakusanya
misemo yote ya salaf. [5]
Al Qurtubee alitaja katika tafseer yake [6], rai ya wale wanaosema
"Kamba ya Allah" inamaanisha Qur'aan, na rai ya wale wanaosema kuwa
inamaanisha Jamaa'ah. Kisha akasema:"Maana iliyokusudiwa hapa
zimekaribiana na zimefanana kwani Mwenyezi Mungu anatuamrisha tuwe
wamoja na kutukataza na kufarikiana. Hii ni kuwa (huko) kufarikiana
ni maangamizi na kushirikiana na Jamaa'ah ni maokovu.
Naye Shaykhul Islaam ibn Taymiyyah akasema: "Kamba ya Mwenyezi
Mungu" imefasiriwa kuwa; Kitabu Chake, Dini Yake, Uislamu, Dhati,
Amri Yake, Agano Lake, Utiifu kwa Allah, na Jamaa'ah. Misemo yote
haya yametajwa na maswahaba na wale waliowafuata katika kutenda mema
mpaka siku ya Kiyama. Na yote haya ni Saheeh, kwani Qur'aan
inatuamrisha juu ya Dini ya Uislamu - na hii ndiyo Amri ya Mwenyezi
Mungu, (vile vile ndilo) Agano lake na Utiifu wa Mola. Na
kushikamana na yote haya kwa ujumla (kwa umoja wa watu)
haitawezekana isipokuwa kwa Jamaa'ah. Na dini ya Uislamu ki uhakika
na kuwa mkweli na wazi kwa Mwenyezi Mungu.
Ibn Jareer at-Tabaree amesema katika tafseer yake [8] kuwa Qataada
amesema kuhusu aya hii "Wala musifarikiane, na mukumbuke baraka ya
Mwenyezi Mungu juu yenu" - Kwa hakika, Mwenyezi Mungu anachukia
kuona kuwa ummah umegawanyika na Anatukataza na jambo hili. Na
anapenda kuona tunatwi'i na kushikamana na Jamaa'ah. Basi pendaneni
baina yenu kwa yale Mwenyezi Mungu anayowapendelea - kiasi cha uwezo
wenu. Na hamna nguvu isipokuwa kwa (amri yake) Mwenyezi Mungu.
Kumbukumbu
1. Neno la mfasiri: Jamaah inakusudia ummah wa waislamu kwa ujumla
walioshirikiana juu ya haki au juu ya mambo ya utawala wa ummah.
2. Tafseer ya Ibn Hateem (2/455) na aliye nukuu hadithi hii ni Abd
Rabihh Ibn Baariq al-Hanafee. Al-Haafidh Ibn Hajar asema kumhusu mtu
huyu:"Yeye ni mwaminifu lakini hufanya makosa (wakati wa kunukuu)"
3. Al-Muharra al-Wajeez fee Tafseer al-Kitaab-il-Azeez (3/182)
(Iliochapishwa na al-Maghrib)
4. Imenukuliwa na Ibn Jareer katika Tafseer yake (4/32), Ibn Haatim
katika tafseer yake (2/452-453) kutoka kwa njia ya Yazeed
ar-Raqaashee kutokamana na Anas, lakini silsila huo ni dhaifu. Hii
hadithi imetolewa kupitia njia nyingi zenginezo kutoka kwa Anas na
wengineo. Misemo yote haya tofauti huongeza nguvu baina ya hii
hadith, isipokuwa haikutajwa miongoni mwa yote haya kutaja aya,
isipokuwa hii riwaya moja tu ya Anas - kulingana na ninavyo elewa.
5. Kuna kauli sita ambazo Ibn al-Jawzee amezitaja katika Tafseer ya
Zaad al-Maseer (1/432) (Imechapishwa na al-Maktab al-Islamee)
6. Al-Jaami' Li-Ahkaam-il-Qura'an (4/159) (Imechapishwa na Dar
Al-Kutub)
7. Minhaaj as-Sunnah (5/134) (Imechapishwa na Jaamiah al-Imaam
Muhammad Ibn Sa'ood al-Islamiyyah)
8. Jaami' al-Bayaan 'an Ta'weel Ayy-il-Qur'aan (4/32)
|
 |
|
|
| |
|
|
|
|
|
|
 |
 |
|
|
|