TAWHIYD
    Tawhiyd

Qur'aan

Sunnah

Fiqhi

Makala

Nasiha Ya Ijumaa

Dua na Adhkaar

'Aqiyda-Tawhiyd

Vitabu

Darsa za Wanawake

    Sikiliza

Qur'aan

Mawaidha

Dua

Nashiyd

    Tizama

Video

 »  Sira  

MABINTI WA MTUME WA MWENYEZI MUNGU (SAW)

 1    Zainab ( RA )
 2    Ruqayah ( Ra )
 3    Fatima ( RA )
 4    Ummu Kulthum( RA )

Mtume wa Mwenyezi Mungu (SA.W) alipata watoto sita kutokana na mkewe wa mwanzo Bibi Khadija binti Khuwaylid (RA), wanaume wawili na wanawake wanne. Watoto wa kiume aliwapa majina ya Qassim na Abdullah aliyekuwa akijulikana pia kwa jina la Al Taher, amma watoto wa kike ni Zeinab na Ruqayyah na Ummu Kulthum na Fatima (RA).

(Zipo riwaya zinazosema kuwa alitangulia Fatima (RA) kisha Ruqayah (RA) na nyingine zinasema kinyume na hiyvo).

 Qassim aliyezaliwa katika mwaka wao wa mwanzo wa kuoana alifariki dunia akiwa na umri wa miaka miwili, na kutokana naye Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) anakajulikana kwa jina la ‘Abal Qassim’, yaani babake Qassim.

Kisha akazaliwa Abdullah aliyefariki pia akiwa mtoto mchanga, kisha Zeinab, kisha Ruqayah aliyefanana sana na mama yake, kisha akazaliwa Ummu Kulthum, kisha akazaliwa Fatima aliyefanana sana na baba yake, hasa katika mwendo na sauti.

Katika mafulululizo wa makala haya nitaeleza kwa ufupi juu ya maisha ya mabinti wane wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW), nikianzia na mkubwa wao kwa umri, Bibi Zeinab, kisha Bibi Ummu Kulthum kisha Bibi Ruqayyah na mwisho Bibi Fatima – Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote kwa pamoja.