|
Thawabu za
kufunga sita Shawwaal hazipatikani ila baada
ya kukamilisha mwezi wa Ramadhaan. Kwa hiyo
kama mtu ana deni la Ramadhaan basi kwanza
alipe deni kisha ndio afunge sita Shawwaal
kwani Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
kasema:
((من صام رمضان ثم أتبعه بست من شوال))
))Atakayefunga
Ramadhaan, kisha akafuatia na Sita za
Shawwal….((
[Muslim, Abu Dawud, Tirmidhi, Ibn Majah,
Ahmad, ad-Daarimiy].
Kwa kutokana
na Hadiythi hiyo tunasema kwamba, yeyote
mwenye deni la Ramadhaan alipe kwanza kisha
ndio afunge Sita Shawwaal na ikiwa siku siku
sita za Shawwaal zimeangukia siku ya
Jumatatu na Alkhamiys atapata thawabu zote
(thawabu za kufunga sita Shawwaal na thawabu
za kufunga Jumatatu na Alkhamiys) kwa nia
hizo kutokana na Hadiyth aliyosema Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم
((إنماالأعمال بالنتات وإنما لكل امرئ ما
نوى))
((Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na
kila mtu atapata kwa mujibu wa kile
alichokusudia)).
Shaykh Muhammad bin Swaalih al-`Uthaymiyn
Fiqhul Ibaadaat Ukurasa No.222 Maktabatul
Iman
|