Anasema Allaah سبحانه وتعالى ((مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُواْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلاَ الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَاللّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاء وَاللّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ))((Waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi)) [Al-Baqarah:105] Kuchukia kwao makafiri kwa kuletwa Mtume wa mwisho Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم na kitabu cha mwisho Qur'aan Tukufu kunawapelekea kufanya kila juhudi kwa kutumia kila aina ya mbinu ili wawapotoshe Waislamu katika 'Aqiydah (Iymani) yao iliyo sahihi na waingie katika upotofu. Vitimbi vyao hivi karibuni ni kutunga kitabu wanachokifafananisha na Qur'aan, inayoitwa 'Al-Furqaan Al-Haqq' (The True Furqaan) ambayo imesambazwa na kuuzwa maeneo mengi. Inasemekana imetolewa huko Kuwait.